Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Utangazaji Tanzania ( TBC) kuanziaa Julai 29, mwaka huu wamekutana Mkoani Morogoro kwa kwa ajili ya kupatiwa mafunzo elekezi ya siku tatu kwa Kamati mbili za Bodi hiyo ambazo ni Kamati ya Ukaguzi na Kamati ya Fedha na Utawala .
Mkurugenzi Mtendaji wa TBC, Clement Mshana, alibainisha hayo Julai 29, mwaka huu alipowakabirisha wajumbe wa Bodi hiyo inayoogozwa na Mwenyekiti wake Profesa Mwajabu Possi.
Kwa mujibu wa Mkurugenzi Mtendaji huyo wa TBC, mafunzo ayo yamekuja wiki mbili baada ya mafunzo mengine kwa wajumbe wa Bodi juu majukumu ya Bodi katika Taasisi hiyo.
Katika mafuno hayo , mgeni rasmi alikuwa ni Mkaguzi wa Ndani Mkuu wa Serikali , Mohamed Mtonga.
Mkurugenzi Mtendaji wa TBC, Clement Mshana akitoa nasaha zake kwa wajumbe wa Bodi ya TBC wakati wa Mkutano wao uliofanyika kuanzia Julai 29,Mkoani Morogoro.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa TBC, Profesa Mwajabu Possi akipokea vitabu vya mwongozo wa ukaguzi kutoka kwa Mkaguzi wa Ndani Mkuu wa Serikali, Mohamed Mtonga.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa TBC, Profesa Mwajabu Possi akiwa na vitabu vya mwongozi wa ukaguzi.
Baadhi ya Wakurugenzi wa Idara za TBC na wajumbe wa Bodi wa wakimsikiliza mgeni rasmi siku ya kufungua mafunzo elekezi ya siku tatu kuanzia Julai 29, 2013.
Mkurugenzi Mtendaji wa TBC, Clement Mshana ( kulia) akibadilishana mawazo na baadhi ya wajumbe wa Bodi hiyo pamoja na Mgeni Rasmi, Mohamed Mtonga ( wapili kutoka kilia).Picha na John Nditi,Globu ya Jamii,Morogoro.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...