Si nyingine bali ni Ngoma Africa band a.k.a FFU ughaibuni,bendi maarufu yenye ngome yake kule Ujerumani,chini ya kamanda wao Ras Makunja,bendi hiyo imefanya kweli siku ya jumapili 28.08.2013 katika maonyesho ya Jambo Seeheim Festival,yaliyofanyika mjini Jugenheim-Seeheim,nchini Ujerumani kuliko ungua shoka mpini ukabaki,kama kawaida yake Ngoma Africa band ilianza kuwasha muziki mkali na kuwatia kiwewe washabiki waliokuwapo katika onyesho hilo,bendi hiyo yenye utajili wa wanamuziki wenye vipaji akiwemo afande Christian aka Chris-B, na yule kijana Jonathan Souza a.k.a Jo Jo. Usikose kupata burudani za FFU at www.ngoma-africa.com au http://www.ngoma-africa.com
Ngoma Africa Band Live at jambo seehim,Germany 28.07.2013.
FFU kazini kwao (mwenye miwani) ni kamanda Ras makunja.
Chipukizi wa FFU alikuapo.
Guitarist Matondo Benda.
Mr.Jo Jo, Mkaanga Chips wa Ngoma AFrica.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 31, 2013

    kazi ndio kwanza inaanza FFU kama kawaida msimu wa joto

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 31, 2013

    kamanda mkuu,jemedari kikosi maalum,mfalme wa Anunnaki empire,Field-mashar Ras Makunja wa FFU

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 31, 2013

    FFU babu kubwa,kamanda tangu kurudishiwa bundi wake mambo yanakwenda mswano na ngome yake ya FFU inazidi kuimarika

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 31, 2013

    maafande wa kikosi maalumu naona wapo gado,ninachowapendea ni kuwa mnakumbuka wajibu wenu wa kuwepo ktk malindo yenu

    ReplyDelete
  5. AnonymousJuly 31, 2013

    maafande wa kimataifa aka ffu ughaibuni,kila penye fujo mnakwenda
    kutuliza

    ReplyDelete
  6. AnonymousJuly 31, 2013

    wazee wa kazi ffu Ngoma Africa band chini ya kamanda mkuu ras makunja wa
    kurusha vya machozi

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...