Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akihutubia wakati akifungua rasmi Mkutano wa Mabunge wa kujadili Sera
za Misitu Barani AFrika, uliofanyika jana jioni kwenye Hoteli ya Hyatt
Kilimanjaro, jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi
wa Baraza la Dunia ya baadaye wa Dunia, 'World Future Council'
Alexandra Wandel,akizungumza wakati wa ufunguzi wa mkutano huo.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
(katikati) akiwa na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro
Nyalandu, (wa pili kulia) Mkurugenzi wa Baraza la Dunia ya baadaye wa
Dunia, 'World Future Council' Alexandra Wandel (wa pili kushoto) na
Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki, Getrude Mongela (kulia)
wakifuatilia moja ya mada zilizokuwa zikitolewa ukumbini hapo kupitia
Screen kwa njia ya TV.
Baadhi
ya Wabunge wakiwa katika chumba cha mkutano huo, kutoka (kushoto) ni
Mbunge wa Kahama James Lembeli, Mbunge wa Mafia, Abdulkarim Shah, Mbunge
wa Iringa Mjini, Mchungaji Peter Msigwa na Mbunge wa Kigoma Kusini,
David Kafulila, wakiwa katika mkutano huo jana.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akizungumza na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu
(katikati) na Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki, Getrude Mongela,
baada ya kufungua rasmi mkutano huo jana jijini Dar es Salaam.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wabunge waliohudhuria Mkutano
Mabunge wa kujadili Sera na changamoto za Misitu Barani Afrika
uliofanyika jijini Dar es Salaam, jana.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...