Na Swahili TV, Washington DC
Chuo Kikuu cha Howard  alichokuwa akisoma mtanzania aliyeuawa  mjini Washington Dc,  marehemu Omary Adam Sykes kinataraji kuuaga mwili wake  leo jioni, viongozi mbalimbali akiwemo meya wa jiji la Washington DC Bwana Gray nao wanatarajiwa kuhudhuria.
Kwa mujibu wa taarifa zilizotufikia Swahili TV shughuli za kumuaga  marehemu zitafanyika katika ukumbi wa Andrew Rankin Memorial Chapel ulio katika kona ya  6th Street  na Howard place na kufuatiwa  sherehe za kukumbuka ya  maisha yake zitakazofanyika katika ukum bi wa Blackburn ambao pia uko katika chuo hicho.
Shughuli za kuuaga mwili huo zimepangwa kuanza saa 12 jioni (takriban muda  wa masaa mawili na nusu toka sasa kwa saa za Tanzania), ambazo habari hizo zinasema Mstahiki meya  Vicent condol Gray atakuwa muongeaji mkuu akishirikia na rais wa chuo hicho  Profesa Sidney A. Ribeau. Sherehe hizi pia zitashirikisha familia ya marehemu Omar ambaye baba yake mzazi mze Adam Sykes  na baba yake mkubwa waliingia jana wakitokea nchini Tanzania.
Si jambo la kawaida kwa Meya wa jiji kubwa la Washington  kuhudhuria sherehe za kuuga mwili, wachambuzi wa mambo ya siasa za Washington Dc  wanasema  hali  hiyo huenda inatokana na umaarufu wa chuo hicho na mstuko mkubwa wa mauaji ya mwanafunzi  huyo ambayo yamelistua jiji la Washington DC,  ambalo licha ya kuwa na matukio ya mauaji ya hapa na pale  lakini eneo la chuo hicho limekuwa salama kwa miaka mingi.
Taarifa ya chuo kwa Swahili TV inasema,Uongozi wa chuo uliamua kuanzisha mfuko maalum utakaosaidia wananchi mbalimbali wasio na uwezo kulipia ada zao, mfuko utatambulika kama Omar Scholarship Fund na tayari watu kadhaa wameshaanza kuchangia.Taarifa za namna ya sifa na uwasilisha wa maombi zitatangazwa baadaye.

Swahili TV itakuwepo katika shughuli za kuuaga mwili ili kukuletea habari za kina na uhakika.

Stay tuned for Exclusive story at www. swahilitv.blogspot.com

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 11, 2013

    Chuo cha nguvu hicho .private na Jamaa atakuwa alikuwa kichwa .R.I.P

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 11, 2013

    inna lillahi waina illahim rajiun may Allah rest his soul in peace amin poleni sana wafiwa, wazazi,ndugu,jamaa na marafiki ndo mwisho wa binadamu

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 11, 2013

    Inna LiLLAh picha inaonesha kijana alikuwa mtulivu what a loss, ila ndio hivyo ALLAh mjuzi wa yote na kazi yake kamwe haina makosa, MAy he Rest in PEace

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 11, 2013

    mdau wa kwanza kuna tafauti ya Havard na Howard. Havard ndio chuo private na cha nguvu, samahani nilihisi nikuzindue tu

    ReplyDelete
  5. AnonymousJuly 11, 2013

    ANONY unayotaka kuzindua watu wewe mwenyewe hujui hata kuandika sahihi, ni HARVARD sio Havard, na chuo cha Howard pia kinajulikana sana, hasa kwa Wamarekani weusi. Jaribu kutumia google na utajua haraka umuhimu wa chuo hicho kwa Wamarekani weusi.

    ReplyDelete
  6. AnonymousJuly 11, 2013

    RIP Omary..so sad to hear!

    Mwandishi ufanye research kabla ya kuandika....Howard si chuo maarufu hapa marekani. Howard ni chuo cha watu weusi na kilianzishwa kuwasaidia watu maskini hasa weusi. Ni chuo ambacho hakina reputation nzuri academically kama ulivyoandika na hata kwenye orodha ya vyuo 100 best vya hapa america hakipo.

    Meya anahudhuria maana eneo lilipotokea ni chini ya utawala wake na viongozi hapa wanathamini sana watu na its very unfortunate kwao kwa mtu hasa kijana kufa bila sababu ya msingi. Huku watu wapo responsible sana.

    mdau
    washington DC

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...