Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwasili Kigogo Mburahati, jijini Dar es Salaam, leo Julai 30, 2013 nyumbani kwa aliyekuwa Mhasibu Mkuu wa Ofisi ya Makamu wa Rais, Juma Haji Mkima, kwa ajili ya kutoa mkono wa pole kwa famili ya mhasibu huyo aliyefariki dunia jana katika Hospitali ya Aga Khan. Marehemu Juma, anatarajia kuzikwa leo kijijini kwao, Rufiji.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimfariji mke wa marehemu Juma Haji Mkina, Kibibi Juma Mkina, aliyekuwa Mhasibu Mkuu wa Ofisi ya Makamu wa Rais, aliyefariki dunia jana katika Hospitali ya Aga Khan, jijini Dar es Salaam. Makamu wa Rais alifika nyumbani kwa marehemu Kigogo Mburahani leo Julai 30, 2013 kwa ajili ua kutoka mkono wa pole, kabla ya marehemu kusafirishwa kwenda kuzikwa kijijini kwao Rufiji.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akijumuika pamoja na waombolezaji nyumbani aliyekuwa Mhasibu Mkuu wa Ofisi ya Makamu wa Rais, Juma Haji Mkina, aliyefariki dunia jana katika Hospitali ya Aga Khan, jijini Dar es Salaam. Makamu alifika nyumbani kwa marehemu Kigogo Mburahati, leo Julai 30 kwa ajili ya kutoa mkono wa pole na kuwafariji wafiwa.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiondoka Kigogo Mburahati, jijini Dar es Salaam, leo Julai 30, 2013 nyumbani kwa aliyekuwa Mhasibu Mkuu wa Ofisi ya Makamu wa Rais, Juma Haji Mkima, baada ya kufika kutoka mkono wa pole na kuwafariji wafiwa kutokana na msiba huo. Marehemu Juma, anatarajia kuzikwa leo kijijini kwao, Rufiji. Picha na OMR.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 30, 2013

    mhasibu mkuu anakaa kigogo umewahi kuona wapi. Huyu ni mtu aliyekuwa anafanya kazi za mamilioni ya dola na hakuwahi kuiba hata mara moja.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 30, 2013


    M/MUNGU AMLAZE MAHALA PEMA PEPONI. ANAONEKANA ALIKUWA MUADILIFU KWA NAFASI YAKE PENGINE MSIBA USINGEKUWA KIGOGO MBURAHATI BADALA YAKE MASAKI/MIKOCHENI/OYSTERBAY NK

    LAKINI MAREHEMU AMEISHI NA WATU WA KAWAIDA NA NYUMBA YA KAWAIDA KABISA

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 30, 2013

    R.I.P CHIEF TUTAKUKUMBUKA DAIMA

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 30, 2013

    Can't believe chief accountant for vice president office live at kigogo is it true????

    ReplyDelete
  5. AnonymousJuly 30, 2013

    BALI KWA KIZAZI CHA SASA MTU KAMA HUYU ANAONEKANA ALIKUWA MJINGA.

    SI HAKUIBA NA KUJENGA HEKALU!!!

    Mungu ibariki Tanzania!

    Ameeen.

    ReplyDelete
  6. AnonymousJuly 31, 2013

    R.I.P ,Ni wengi sana wenye kustaajabu yaliyokua makazi wakati wa uhai wake marehemu Mkina,Hii ni picha halisi iliyopo ktk jamii yetu ya kitanzania kwa sasa yenye kuakisi uwazi/ufa/gepu kubwa kati ya wao na sisi au wenye nacho na wasio nacho,katika hali ya kawaida wadhifa,kipato, elimu au hata kuruka hewani sana si sababu ya kuacha kuishi baadhi ya maeneo(Maarufu kama Uswazi),lakini leo jamii imepokea na kukubari kasumba hii kwa kiasi cha baadhi ya watu kama huyu na wengineo kuonekana kama wa ajabu,Ktk kumbukumbu zangu hapahapa bloguni kuna mdao mmoja aliyejitamburisha kama mfanyakazi wa Mamlaka ya mapato(TRA)alikua anaomba msaada arudishiwe vitambulisho vyake vilivyoibiwa akiwa ndani ya daladala akirudi nyumbani kwake Mwananyamala, yule bwana alishambuliwa sana na watu kwa kuonekana mjinga eti kwanini bado anapanda daladala ilihali yupo TRA?Walikuwepo wengine waliokwenda mbali zaidi kwa kusema mganga wake kampa masharti magumu ya kupanda daladala tu vinginevyo kibarua kitaota nyasi,Jamii haikubariani na kile inachokiona kwakua mfumo umeharibika.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...