Na Mdau wa globu ya jamii.
Wanachama wa RAAWU Tawi la Makumbusho ya Taifa nchini, wameitimua safu yote ya uongozi wa Tawi la chama hicho kwa kile kinacho elezewa kushindwa kutekeleza majukumu yao ya kutetea wafanyakazi wa Shirika hilo pale wanapo kandamizwa na mwajiri wao.
Wakitoa malalamiko yao mbele ya uongozi wa RAAWU kanda ya Mashariki ulio ongozwa na Bw Joseph Sayo, wajumbe wa tawi hilo la Makumbusho hapa nchini walisema kuwa ni mara kadhaa sasa mwenyekiti wa Dkt Amandus Kweka ameshindwa kuwatetea kwenye vikao vya menejimenti hasa pale mwajiri anapo jadili mambo yanayo onesha wazi wazi kuwakandamiza wafanyakazi kitu kinacho sababisha migangano ya mara kwa mara kati ya wafanyakazi wa Shirika hilo na Uongozi wao.
Baadhi ya malalamiko yaliyo tolewa na wanachama hao ni pamoja na Mwenyekiti wao Dkt Kweka kushindwa kuwatetea wafanyakazi walio fukuzwa kazi kwa uonevu, na alibariki mkataba ulio takiwa kusainiwa na akina dada wawili (majina tumeyahifadhi) ambao ni wafanyakazi wa Makumbusho ya Taifa wenye kipengele cha kuwazuia kuolewa pindi wanatakapo kuwa masomoni na hata watakapo rudi kazini kwa muda maalumu uliopo katika mkataba huo, jambo ambalo lililaaniwa na kila mwana RAAWU wa Makumbusho ya Taifa.
Mambo mengine ni pamoja na Mwenyekiti huyo kuto kuteteha stahili zao za msingi kama posho za muda wa siada na ule wa kawaida wa kazi, wamesema kuwa wamekuwa mara kwa mara wakifanya kazi bila ya kulipa malimbikizo yao hali inayo wapelekea kuendelea kuwa na maisha magumu angali wakiwa na watu wanao wategemea katika familia zao.
Wanachama hao wa RAAWU tawi la Makubusho ya Taifa hapa nchini waliouomba uongozi wa chama hicho kanda ya Mashari kusiaidia kufuatilia tatizo la shirika hilo kuongozwa na Makaimu wa Kurugenzi na kutokuwa na Bodi ya Shirika kwa miaka kadhaa sasa, hali inayo pelekea kutokuwa na chombo kamili chenye madaraka ya kutatua matatizo yao kwa urahisi na haraka.
Akijibu baadhi ya tuhuma zilizo kuwa zikimkabili Mwenyekiti wa RAAWU tawi la makumbusho Dkt Amandus Kweka alikanusha na kumesama kuwa hata siku moja katika uongozi wake haujawahi kushiriki katika maamuzi yanayo mkandamiza mfanyakazi, bali amekuwa akijitahidi sana kuwatetea, na akatoa mifano kadhaa ya wafanyakazi walio tetewa na kupata haki zao pale zilipo taka kuporwa na muajiri.
Dkt Kweka aliongeza kwa kuulaumu uongozi wa juu wa shirika hilo Ulio simamishwa kwa tuhuma mbali mbali ya matumizi mabaya ya Ofisi kuwa ulikuwa ukifanya maamuzi ya kuwakandamiza wafanyakazi bila ya yeye kushirikishwa katika kupitisha maamuzi hayo. Hata ihivyo aliwataka wanachama wa tawi hilo kuto kuwa na jazba pale wanapo ona kuwa hawajatendewa haki bali wafuate utarabu wakuwashirikisha viongozi wao wa chama ili kupata utetezi stahili.
Akizungumza na wanachama wa Makubusho ya Taifa nchini, Katibu wa RAAWU kanda ya Mashariki Bwana Joseph Sayo amewataka viongozi wote wa Matawi kanda ya Mashariki kususia vikao vinavyo onesha wazi wazi kuwa nahoja ya kuwakandamiza wafanyakazi ili kuonesha wazi kuto kukubaliana na maamuzi hayo ya Muajiri ili kuwasaidia wafanyakazi wa Taasisi zilizo chini ya mwamvuli wa RAAWU hapa nchini. Amewashauri wanachama kuwa ndio wanye nafasi ya kumng’oa kiongozi yeyote mwenye kushiriki katika maamuzi ya manejimenti yanayo wakandamiza wafanyakazi na kumfaidisha muajiri.
Hata hivyo Bwana Sayo amesema chama hakina mgogoro na waajiri na kitakuwa tayari kushirikiana na waajiri kwenye mambo ya msingi na kuto kukubaliana kwenye mambo yasiyo na maslai kwa wafanyakazi, ili kuepusha migogoro makazini, na kwa upande wa wawafanyakazi Katibu wakanda ya Kaskazini amesema RAAWU haitasita kushirikiana na mwajiri kumwadhibu mtumishi anapo kiuka taratibu na kanuni za kazi ili kulinda heshma ya chama.
Wanachama wa RAAWU tawi la makumbusho walikutana na Uongozi wa kanda ya Mashariki na kufikia maamuzi hayo ya kuutimua uingozi wa RAAWU tawi na kukubaliana kuunda kamati maalum itayayo ratibu na kusimamia uchaguzi wa viongozi wapya wa Tawi hilo haraka iwezekanavyo. Wajumbe wa kamati hiyo ni pamoja na Achiles Bufure Marugisu Filip, Irene Mville, Agnes, Prisca Mangazini.
Hao makumbusho wana matatizo gani? Tuu much majungu shirika halitawaliki. Ona sasa viongozi wote hamna. Bodi wakurugenzi na sasa Mwenyekiti RAAWU.
ReplyDeleteSio majungu wala nini. Shirika litatawalika tu endapo mihimili inayoongoza shirika itakuwepo. tunataka viongozi wenye mamlaka kamili (Bodi, Mkurugenzi Mkuu na Wakurugenzi)
ReplyDeleteMapambano bado yanaendelea, hadi kieleweke...
Nivizuri viongozi wajue thamani ya wafanyakazi, si vizuri kuwa kuwanyima stahili zao, hata hivyo tunasikia shirika hilo linaelekeza pesa zaidi kwenye mambo ambayo si ya kimakumbusho, na kuviacha vituo vikihangaika tu. Serikali kuu yapaswa kuingilia kati sasa maana shirika hili ndilo mkombozi wa Urithi wa Taifa hili ya vyote vinavyodhaminiwa wa watanzania. MAKUMBUSHO NDIO NCHI, naomba ifahamike hivyo, na si sehemu ya kuchezewa chezewa kama hivi sasa.
ReplyDeleteHuyo wafanyakazi wana mamlaka ya kumuondoa. Mamlaka ya wafanyakazi wangeruhusu hata uongozi mzima wa shirika tungeung'oa. Serikali imeweka kando mambo mengi ya shirika hili, wengine wanawekwa kando kupisha uchunguzi, miaka inakatika na hakuna kinachoendelea na kufaidi mshahara na stahili zote kama kiongozi. INASIKITISHA SANA
ReplyDeleteNyie MAKUMBU namnagani bana, Mbona kama hamtambuliwi na Wizara yenu, Mnaonekana kuwa mnatunza tu vitu vya zamani hadi Uongozi unamambo ya kizamani. Ukabila umetawala sana hapo, mambo yenu Kich..g.. kikaskazini tu. Pesa zote za shirika manataka ziamie KLM. Hebu kaaeni mjitafakari na kuachana na tabia za ukabila na udini, toeni kipaombele kwenye mambo ya msingi ili kuendeleza shirika, shirika hilo ni lawatanzania si lenu. Mnashindwa hata kuwajulisha watanzania mambo mnayo fanya humo (Kulitangaza shirika kitaifa na Kimataifa) kwa maana mnambambo yenu yasiyo faa. Waziri alijitahidi kutatua kero sasa walio letwa wanaonekana wameshondwa kuliendeleza shirika. POLE MAKUMBUSHO YA TAIFA.
ReplyDelete