IMG_1336
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala Jerry Silaa akizungumza na uongozi wa Al Madrassatul Munauwaratul Islamiya iliyopo Msasani Bonde la Mpunga Ofisini kwake leo jijini Dar es Salaam wakati wa hafla fupi ya kukabidhi Spika mbili, Vipaza sauti viwili (Microphones) pamoja na Amplifaya ambavyo vitatumika kuendeshea shughuli mbalimbali za kueneza mafunzo ya dini kwa jamii na watoto wanaosoma chuoni hapo. Vifaa hivyo vimetolewa na mdau mpenda maendeleo kupitia kwa Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala Jerry Silaa.
IMG_1339
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala Jerry Silaa pamoja na Bw. Abdulmalik Ibrahim (kulia) aliyemwakilishi mdau aliyetoa vifaa hivyo (jina kapuni) wakikabidhi Spika tatu, vipaza sauti viwili na Mixer kwa Katibu wa Madrasa hiyo Bw. Salim Amri (wa pili kushoto) aliyeambatana na Ustaadh Nurdin Nassor Abdallah (katikati). Kushoto ni mmoja wa walimu wa madrassatul Munauwaratul Islamiya kilichopo Msasani Bonde la Mpunga Ustaadh Mohamed Kassim.
IMG_1344
Mstahiki Meya Jerry Silaa akikagua moja vifaa hivyo alivyokabidhi leo ofisini kwake .
IMG_1360
Ustaadh Nurdin Nassor Abdallah wa Al Madrassatul Munauwaratul Islamiya ya Msasani Bonde la Mpunga akitoa shukrani kwa Mstahiki Meya Jerry Silaa pamoja na mdau alijitolea baada ya kupokea vifaa hivyo ambavyo amesema vitawasaidia katika kazi zao za kueneza neno la Mungu hasa kipindi hichi cha mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhani ikiwemo kuhubiri Amani nchini.
IMG_1372
Uongozi wa Al Madrassatul Munauwaratul Islamiya kilichopo Msasani Bonde la Mpunga wakiomba dua za baraka kwa msaada waliopokea leo ofisini kwa Mstahiki Meya Jerry Silaa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 29, 2013

    Jina kapuni?? hilo jibu linatoka kwako, wewe wakuitwa misupu au la huyo mwakilishi!!

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 30, 2013

    Is Jerry a muslim, why pretend praying? siasa iko kazi.

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 30, 2013

    Msemaji wa pili hebu elimika kidogo. Wakati wa kuomba kwenye jumuia sote huwa tunamuomba Mungu. Pale sala inapanda kama kawa. Unweza kuomba kwa staili yoyote, ilmradi usimkashifu Muumba wetu

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 30, 2013


    MSAADA ATOE MWINGINE CREDIT ANACHUKUA MWANASIASA!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...