Serikali imekuwa ikipiga vita sana kuchomwa kwa misitu katika maeneo mbali mbali hapa nchini,lakini kauli hiyo imeonekana kuwa kama haina nguvu sana kwenye maeneo mengi ya vijijini,kwani zoezi la kuchoma moto misitu na kuzalishwa magunia kwa maginia ya mkaa imekuwa ikichukua nafasi kubwa siku hadi siku.Kikubwa kinachostaajabisha ni pale kauli ya Serikali inapokuwa inapingana na baadhi ya watendaji wake,kwani kuna maeneo mbali mbali humo njiani kuna vituo vya kukusanya ushuru wa mkaa huu huu.....!!!ambao wateja wake wakubwa ni wakazi walio katika maeneo ya mijini.sasa nini kifanyike kuhakikisha misitu yetu inatunzwa na haichomwi tena??

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 06, 2013

    Wachina nao wanavuna tuu mbao kama zao, haya huku nao wauza mkaa wameshika kasi,Yoote haya ni sababu ya rushwa rushwa rushwa, iwapo kama kusingekua na rushwa basi uthibiti wa biashara ya magogo tunayopigwa bao na wachina pamoja na hili la mkaa linalofanywa na wananchi ungepungua kama si kwisha kabisa.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 06, 2013

    Jana nilitembelea maonyesho ya sabasaba Daresalaam,kuna banda(jina nimelisahau)karibu na banda la MALIASILI na UTALII,pale kuna njia nyingi na nzuri za nishati mbadala(Kwa mnaoingia kwenye maonyesho haya,nendeni pale mpate maelezo),wakti mwingine tunahitaji kuisaidia serikali.Wale wenye banda lile wanastahili kusamehewa kodi na wasambaze bidhaa zao nchi nzima,ikiwemo na kuelimisha wananchi.Tunaweza kuanzia majaribio mijini kwanza.

    David V

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 06, 2013

    ifike mahala watanzania tuwe na uchungu na hazina kubwa ya msitu tuliopewa na mwenyezi mungu tusione kana kwambwa upo tu hauishi na utaendelea kuwepo sijui serikali ina mpango gani kuhusu misitu yetu,pesa za Rais wa dunia Barrack Obama zifanye kazi iliyokusudiwa na imani umeme ukufika mpaka vijijini wimbi hili la kutafuna msitu litapungua kama siyo kuisha kabisa.

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 06, 2013

    Nani hajawahi kutumia mkaa nyumbani kwake au kula chakula kilichopikwa kwa mkaa? Gesi inapatikana Mtwara lakini tusishangae watu wengi wakashindwa kumudu gharama yake na kuendelea kukata miti.

    ReplyDelete
  5. AnonymousJuly 06, 2013

    Hivi mnaongea tuu bila kutafakari huyu mtu unaemwambia asitumie mkaa unategemea atumie nini??????? mimi nina gas lakini nikiona inaisha pressure inapanda nitajaza na nini huyo mtungi kamshahara kangu kadogo. Mafuta ya taa siyamudu hata kidogo mara nyingi najiuliza huyu mwananchi ambaye anaishi maisha ya kubangaiza anamuduje kwani nishati ziko juu sana angalau mkaa ni afadhali kidogo. Tupeni altenative sio tu kuzuia kwani tangu nimezaliwa kijijini kwetu tulikuwa tunatumia kuni kutoka kwenye misitu iliyotuzunguka na mikaa TUNACHOOMBA NI ALTENATIVE. Nimejitahidi nikanunua hayo majiko tunaambiwa yanatumia mikaa ya kutengenezwa na makatatasi na mabua lakini yote ni vioja tupu kwenye maonyesho utaona kama ni kitu kitakachosaidia ingia kwenye utendaji hakuna lolote. Gas 54000 mtungi mshahara 150000 embu piga picha hapo! where are we heading to ???????????????

    ReplyDelete
  6. AnonymousJuly 06, 2013

    Tuache porojo,Nani nyumbani kwake hatumii mkaa? na kwanini tunatumia? haya ndiyo maswali ya kujiuliza na tukiweza kuyapatia ufumbuzi huo mkaa hautakuja mjini.
    Isitoshe Serikali inatoa kibali cha ukataji,hii inatoa picha kuwa wanatambua swala la nishati ya mkaa.
    Kiufupi gharama za nishati ziko juu sana kiasi ambacho kwa mtu wa kawaida ni vigumu kwa mtu kununua gesi ama kutumia umeme.
    Mkaa ndiyoo kimbilio letu kwa kipato cha kati na cha chini hilo halikwepeki na tena kwa jinsi sasa hivi maisha yalivyokaza basi hata wale cha juu wataanza/wameshaanza kutumia na ndiyo maana unaona unakuja kwa wingi mujini.

    ReplyDelete
  7. AnonymousJuly 06, 2013

    PLEASE!!!!!!!!,

    1.Remember CET (Clean Energy Technology)

    2.Remember CDM (Clean Development Mechanism)

    3.Remember GLOBAL CLIMATE CHANGE!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...