Ujenzi wa Barabara ya Kutoka Songea mjini mpaka Wilaya Namtumbo Mkoani Ruvuma,umeonekana kwenda vizuri sana pamoja na kwamba ni sehemu kidogo tu imebakia ili imalizike kabisa.Barabara hiyo ambayo hapo awali ilikuwa ikipitika kwa shida sana (kwa mujibu ya wakazi wa miji ya barabara hiyo) hasa wakati wa kipindi cha Mvua,lakini sasa imekuwa ni tofauti kwani imeweza kuziunganisha Wilaya hiyo kwa urahisi.pichani ni baadhi ya Mafundi wa Kampuni ya Sogea wakiwa kazini mchana wa leo.
 Moja ya Mitambo ya Kutengenezea Barabara,likiendelea na kazi yake.
 Mafundi kazini.
 Jamvi la maana kama linavyoonekana pichani.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 19 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 16, 2013

    Bravoooooo.Hyo Kampuni ya SOGEA(Kama ilivyoandikwa) ni ya wazawa?Naomba majibu kwa anayefahamu, kuna "nondo" nataka kuzishusha.

    David V

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 16, 2013

    Hiyo barabara ni ya kiwango cha chini sana, mhh unbelievable kwamba bado barabara zinajengwa katika mjengo huo, sasa ikinyesha mvua ya nguvu si barabara yote inazolewa

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 16, 2013

    KWA NINI WANAJENGA NJIA MOJA TU? NI LAZIMA KUONA YA MBELE NA KUANZA KUJENGA NJIA TATU ZA KWENDA UPANDE MMOJA NA NJIA TATU ZA KURUDI.

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 17, 2013

    Mkeka wa nguvu?yawezekana ikawa ni picha tu,yumkini rahisi hata kukindua hiyo rami kwa kisigino, subiri makabidhiano ndio tuseme.

    ReplyDelete
  5. AnonymousJuly 17, 2013

    tatizo hilo jamvi ni kama majamvi mengine , yakishatandikwa ndio imetoka mpaka liamba, angalia mfano barabara za dar mjini zilikuwa jamvi miaka kama mitano iliopita tukasema yeees na sisi tupo , sasa hivi yametoboka yote hata ukimtia tembo basi atapenya.

    ReplyDelete
  6. AnonymousJuly 17, 2013

    Barabara ni kama mke vile, lazima umtunze atunzike,usipompiga soap soap basi anachujika na hapendezi tena, barabara matunzo, usione vinaelea vimeundwa, "If the grass is greener on the other side, you can bet that the water bills are higher too"

    ReplyDelete
  7. AnonymousJuly 17, 2013

    wadau na nyie mnamaneno, 3 za kwenda na 3 za kurudi huko namtumbo wakati huko lyandembwela hakuna barabara ni matope tu hivyo tunasubiri wamalize hiyo wahamie huku maana mvua ikinyesha hakupitiki. Kwakweli, hii awamu kama ni barabara zimejengwa tunashukuru kwa kazi hiyo nzuri lakini mashaka yangu ni ktk suala la ubora maana hata Dr. Magufuli simsikii tena kama kakata tamaa hivi! Kaona mwajili wake hamsapoti naye kaamua kunyamaza ziliwe za wakora. Kama ubora unazingatiwa basi Mhe. JK 2015 tuta msend off kwenda zake kupumzika kule Goba au Manelamango akiwa ameacha legacy nzuri kwa upande wa miundombinu hilo halina ubishi. Hata ile barabara ya kule Iringa-Dom (JK Drive) inakaribia kuisha, Sumbawanga -Mbeya nayo inawakandarasi 3, huko kaskazini nako usiseme, asate JK. Tunaomba pia kabla yakuondoka airpot ya kisasa ijengwe hapo termina 3 au huko Mkuranga kama sehemu ya utekelezaji wa mkakati wa big result now.

    ReplyDelete
  8. AnonymousJuly 17, 2013

    Tatizo lenu mnaongea tu wakati hata taaluma yenyewe hamna, angalie hiyo thickness kwenye hizo picha za juu utapata majibu ni lami ya aina gani, inaonekana ni imara, sio zile za kunyunyizia mchuzi juu kam mnazoziona sehemu nyingi ya barabara za pembezoni, hasa dar. Mfano, uhuru road, Lumumba n.k. Kwa mdau wa kwanza Sogea ni kampuni ya nje na imefanya kazi nyingi kama hizo hapa bongo.

    ReplyDelete
  9. AnonymousJuly 17, 2013

    Kwa Tanzania, barabara za kwenda Mikoani, "One Lane" inatosha. Moja ya kwenda, na moja ya kurudi. Hatuna magari mengi hivyo, kuhitaji kuwa na "Three Lanes".

    ReplyDelete
  10. AnonymousJuly 17, 2013

    Kama ingekuwa ni amri yangu, ingeanza kwanza barabara ya kutoka Tunduru hadi Namtumbo halafu hii ingefuata. Kwa wanaojua shughuli ya kipande cha kutoka Namtumbo kwenda Tunduru, kipindi cha masika, watakubaliana na mimi. Kipande na Namtumbo Songea kwa mtazamo wangu kingeweza kusubiri ili barabara ya Tunduru-Namtumbo kitengenezwe ili kuwaokoa watu wa Tunduru.Labda wamefanya kwa heshima ya Marehemu, Waziri Mkuu wa zamani Ndg. Rashid Kawawa.

    ReplyDelete
  11. AnonymousJuly 17, 2013

    Mkeka wa nguvu ikija siku kukulaza utajuwa kweli mkeka. Hii barabara bilasha inayo ubora. Wito kwa madereva msije jiachia kupita mipaka ya sheria za barabarani kwani huu mkeka unauona wa nguvu basi utakutoa roho kwa nguvu sio mbali.

    ReplyDelete
  12. AnonymousJuly 17, 2013

    Mimi nimetumia barabara hiyo kabla ya ujenzi na wakati ujenzi ukiendelea miaka miwili iliyopita. Ninasikitika kuona mpaka sasa ujenzi haujakamilika. Mwanzoni nilikuwa ninaona kama ujenzi unakwenda vizuri lakini kwa sasa ninamshaka. Kampuni si ya kitanzania, ni ya kigeni, nadhani Ufaransa. Walikuja na mkwara wa vifaa kwel! Mwezi mmoja uliopita nimewakuta wanakarabati kipande cha barabara ya Arusha Minjingu kati ya Arusha na Makuyuni nikadhani hii ya Namtumbo imekwisha!

    sesophy

    ReplyDelete
  13. AnonymousJuly 17, 2013

    Acheni kila mmoja afanye fani yake, hamna kazi ila kunanga wenzenu tu? Nakubaliana na aliyesema barabara inatakiwa soap soap. Nashauri pia madereva pia wapigwe darasa la namna ya kutumia barabara hizi za kisasa na siyo bora liende wabongo.

    ReplyDelete
  14. AnonymousJuly 17, 2013

    Big up JK we are seeing the big result now...

    ReplyDelete
  15. AnonymousJuly 17, 2013

    Angalau si haba!

    Tusitoe lawama na kejeli peke yake, tuangalie huko tulikotoka wakati njia zikiwa ni za ng'ombe na Madaraja ya Mabati tuliyoachiwa na Mkoloni na sasa angalau tuna bararaba zinazopitika kama hizo.

    ReplyDelete
  16. AnonymousJuly 17, 2013

    tattizo niliogundua watanzania wengi hawajuhi nini kinachoendelea duniani wao kutwa kulalamika tu,unataka barabara tatu namtumbo wakati hata dar zenyewe hakuna.watu hawaelewi hata ukubwa wa nchi yao ni kwamba kmsquare ngapi naitatumia pesa ngapi kuweka Rami angarau barabra kubwa za kuonganisha miji.

    ReplyDelete
  17. AnonymousJuly 17, 2013

    SOGEA ni kampuni ya WAFARANSA.

    ReplyDelete
  18. AnonymousJuly 17, 2013

    Corner kali sana hii. karakana ya majeneza yahitajika pembeni! L Mrekebishe na Mungu atatunusuru

    ReplyDelete
  19. AnonymousJuly 18, 2013

    SOGEA SATOM ndo jina la kampuni na ni ya Wafaransa.
    Tangu niifahamu hii kampuni huko Songea ni mara ya pili baada ya kwanza kukutana nao walipokuwa wanapanua Zanzibar airport.
    Kweli Zanzibar kazi nzuri ila hii ya Songea ninamashaka nayo.
    Hiyo ni picha tu lkn japo si mtaalamu na ujenzi, kiwango cha lami hii kwangu mimi ni hafifu. Hii nalinganisha na miradi mingine niliyotembelea kama Laela-Sumbawanga, Daraja mbili(kona za Ruaha)-Iringa na sasa inaendelea mpaka Mafinga kwa uchache. Huko makuyuni sijatembelea ila rafiki yangu amenieleza mambo ni yale yale.
    Wito wangu kwa wahandisi washauri kwenye hii miradi wafanye kazi zao wakiweka uzalendo mbele.
    Maana hawa ndo wanaotuangusha ili hali tunawalipa kwa kodi zetu.
    Hivi majuzi nilipita kwenye mradi unaoanzia Peramiho kwenda Mbinga, nilijaribu kumtafuta mwandisi anipe darasa juu ya daraja moja ambalo halikuniridhisha lkn sikumpata. Nikipita tena nitawajulisha kulikoni.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...