Ujenzi wa Barabara ya Kutoka Songea mjini mpaka Wilaya Namtumbo Mkoani Ruvuma,umeonekana kwenda vizuri sana pamoja na kwamba ni sehemu kidogo tu imebakia ili imalizike kabisa.Barabara hiyo ambayo hapo awali ilikuwa ikipitika kwa shida sana (kwa mujibu ya wakazi wa miji ya barabara hiyo) hasa wakati wa kipindi cha Mvua,lakini sasa imekuwa ni tofauti kwani imeweza kuziunganisha Wilaya hiyo kwa urahisi.pichani ni baadhi ya Mafundi wa Kampuni ya Sogea wakiwa kazini mchana wa leo.
Moja ya Mitambo ya Kutengenezea Barabara,likiendelea na kazi yake.
Mafundi kazini.
Jamvi la maana kama linavyoonekana pichani.
Bravoooooo.Hyo Kampuni ya SOGEA(Kama ilivyoandikwa) ni ya wazawa?Naomba majibu kwa anayefahamu, kuna "nondo" nataka kuzishusha.
ReplyDeleteDavid V
Hiyo barabara ni ya kiwango cha chini sana, mhh unbelievable kwamba bado barabara zinajengwa katika mjengo huo, sasa ikinyesha mvua ya nguvu si barabara yote inazolewa
ReplyDeleteKWA NINI WANAJENGA NJIA MOJA TU? NI LAZIMA KUONA YA MBELE NA KUANZA KUJENGA NJIA TATU ZA KWENDA UPANDE MMOJA NA NJIA TATU ZA KURUDI.
ReplyDeleteMkeka wa nguvu?yawezekana ikawa ni picha tu,yumkini rahisi hata kukindua hiyo rami kwa kisigino, subiri makabidhiano ndio tuseme.
ReplyDeletetatizo hilo jamvi ni kama majamvi mengine , yakishatandikwa ndio imetoka mpaka liamba, angalia mfano barabara za dar mjini zilikuwa jamvi miaka kama mitano iliopita tukasema yeees na sisi tupo , sasa hivi yametoboka yote hata ukimtia tembo basi atapenya.
ReplyDeleteBarabara ni kama mke vile, lazima umtunze atunzike,usipompiga soap soap basi anachujika na hapendezi tena, barabara matunzo, usione vinaelea vimeundwa, "If the grass is greener on the other side, you can bet that the water bills are higher too"
ReplyDeletewadau na nyie mnamaneno, 3 za kwenda na 3 za kurudi huko namtumbo wakati huko lyandembwela hakuna barabara ni matope tu hivyo tunasubiri wamalize hiyo wahamie huku maana mvua ikinyesha hakupitiki. Kwakweli, hii awamu kama ni barabara zimejengwa tunashukuru kwa kazi hiyo nzuri lakini mashaka yangu ni ktk suala la ubora maana hata Dr. Magufuli simsikii tena kama kakata tamaa hivi! Kaona mwajili wake hamsapoti naye kaamua kunyamaza ziliwe za wakora. Kama ubora unazingatiwa basi Mhe. JK 2015 tuta msend off kwenda zake kupumzika kule Goba au Manelamango akiwa ameacha legacy nzuri kwa upande wa miundombinu hilo halina ubishi. Hata ile barabara ya kule Iringa-Dom (JK Drive) inakaribia kuisha, Sumbawanga -Mbeya nayo inawakandarasi 3, huko kaskazini nako usiseme, asate JK. Tunaomba pia kabla yakuondoka airpot ya kisasa ijengwe hapo termina 3 au huko Mkuranga kama sehemu ya utekelezaji wa mkakati wa big result now.
ReplyDeleteTatizo lenu mnaongea tu wakati hata taaluma yenyewe hamna, angalie hiyo thickness kwenye hizo picha za juu utapata majibu ni lami ya aina gani, inaonekana ni imara, sio zile za kunyunyizia mchuzi juu kam mnazoziona sehemu nyingi ya barabara za pembezoni, hasa dar. Mfano, uhuru road, Lumumba n.k. Kwa mdau wa kwanza Sogea ni kampuni ya nje na imefanya kazi nyingi kama hizo hapa bongo.
ReplyDeleteKwa Tanzania, barabara za kwenda Mikoani, "One Lane" inatosha. Moja ya kwenda, na moja ya kurudi. Hatuna magari mengi hivyo, kuhitaji kuwa na "Three Lanes".
ReplyDeleteKama ingekuwa ni amri yangu, ingeanza kwanza barabara ya kutoka Tunduru hadi Namtumbo halafu hii ingefuata. Kwa wanaojua shughuli ya kipande cha kutoka Namtumbo kwenda Tunduru, kipindi cha masika, watakubaliana na mimi. Kipande na Namtumbo Songea kwa mtazamo wangu kingeweza kusubiri ili barabara ya Tunduru-Namtumbo kitengenezwe ili kuwaokoa watu wa Tunduru.Labda wamefanya kwa heshima ya Marehemu, Waziri Mkuu wa zamani Ndg. Rashid Kawawa.
ReplyDeleteMkeka wa nguvu ikija siku kukulaza utajuwa kweli mkeka. Hii barabara bilasha inayo ubora. Wito kwa madereva msije jiachia kupita mipaka ya sheria za barabarani kwani huu mkeka unauona wa nguvu basi utakutoa roho kwa nguvu sio mbali.
ReplyDeleteMimi nimetumia barabara hiyo kabla ya ujenzi na wakati ujenzi ukiendelea miaka miwili iliyopita. Ninasikitika kuona mpaka sasa ujenzi haujakamilika. Mwanzoni nilikuwa ninaona kama ujenzi unakwenda vizuri lakini kwa sasa ninamshaka. Kampuni si ya kitanzania, ni ya kigeni, nadhani Ufaransa. Walikuja na mkwara wa vifaa kwel! Mwezi mmoja uliopita nimewakuta wanakarabati kipande cha barabara ya Arusha Minjingu kati ya Arusha na Makuyuni nikadhani hii ya Namtumbo imekwisha!
ReplyDeletesesophy
Acheni kila mmoja afanye fani yake, hamna kazi ila kunanga wenzenu tu? Nakubaliana na aliyesema barabara inatakiwa soap soap. Nashauri pia madereva pia wapigwe darasa la namna ya kutumia barabara hizi za kisasa na siyo bora liende wabongo.
ReplyDeleteBig up JK we are seeing the big result now...
ReplyDeleteAngalau si haba!
ReplyDeleteTusitoe lawama na kejeli peke yake, tuangalie huko tulikotoka wakati njia zikiwa ni za ng'ombe na Madaraja ya Mabati tuliyoachiwa na Mkoloni na sasa angalau tuna bararaba zinazopitika kama hizo.
tattizo niliogundua watanzania wengi hawajuhi nini kinachoendelea duniani wao kutwa kulalamika tu,unataka barabara tatu namtumbo wakati hata dar zenyewe hakuna.watu hawaelewi hata ukubwa wa nchi yao ni kwamba kmsquare ngapi naitatumia pesa ngapi kuweka Rami angarau barabra kubwa za kuonganisha miji.
ReplyDeleteSOGEA ni kampuni ya WAFARANSA.
ReplyDeleteCorner kali sana hii. karakana ya majeneza yahitajika pembeni! L Mrekebishe na Mungu atatunusuru
ReplyDeleteSOGEA SATOM ndo jina la kampuni na ni ya Wafaransa.
ReplyDeleteTangu niifahamu hii kampuni huko Songea ni mara ya pili baada ya kwanza kukutana nao walipokuwa wanapanua Zanzibar airport.
Kweli Zanzibar kazi nzuri ila hii ya Songea ninamashaka nayo.
Hiyo ni picha tu lkn japo si mtaalamu na ujenzi, kiwango cha lami hii kwangu mimi ni hafifu. Hii nalinganisha na miradi mingine niliyotembelea kama Laela-Sumbawanga, Daraja mbili(kona za Ruaha)-Iringa na sasa inaendelea mpaka Mafinga kwa uchache. Huko makuyuni sijatembelea ila rafiki yangu amenieleza mambo ni yale yale.
Wito wangu kwa wahandisi washauri kwenye hii miradi wafanye kazi zao wakiweka uzalendo mbele.
Maana hawa ndo wanaotuangusha ili hali tunawalipa kwa kodi zetu.
Hivi majuzi nilipita kwenye mradi unaoanzia Peramiho kwenda Mbinga, nilijaribu kumtafuta mwandisi anipe darasa juu ya daraja moja ambalo halikuniridhisha lkn sikumpata. Nikipita tena nitawajulisha kulikoni.