Rais Mstaafu wa Marekani, George Bush (kushoto) akiwa na baadhi ya watoa mada katika Mkutano wa Wake wa Marais Afrika, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC, Mizinga Melu (kulia) na Mkurugenzi Mtendaji wa VIA Aviation, Susan Mashibe, jijini Dar es Salaam jana. Mkutano huo wa siku mbili ulimalizika jana.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) Mizinga Melu (wa pili kushoto) akitoa mada kuhusu maendeleo ya wanawake viongozi wakati wa Mkutano wa Wake wa Marais wa Afrika jijini Dar es Salaam jana. Kutoka kushoto ni Balozi Mark Green Rais na Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Global Development (IGD), Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Group Loid Engenharia SGPS, Loide Monteiro na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya VIA Aviation, Suzan Mashibe.
Rais wa zamani wa Marekani, George Bush (wa pili kushoto) akiwa na baadhi ya watoa mada kuhusu maendeleo ya wanawake viongozi wakati wa Mkutano wa Kimataifa wa Wake wa Marais wa Afrika jijini Dar es Salaam jana. Kulia kwake ni Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC, Mizinga Mwelu na kulia kwake ni Mtendaji Mkuu Kampuni VIA Aviation, Susan Mashibe. Wengine ni maofisa wa NBC, kutoka kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Sheria, Clara Rubambe na kutoka kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Rasilimali Watu, Flora Lupembe na Mkurugenzi wa Masoko na Mawasiliano wa benki hiyo, Mwinda Kiula Mfugale.
Rais Mstaafu wa Marekani, George Bush (kulia) akipozi kwa picha na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC Tanzania , Mizinga Melu wakati wa Mkutano wa Wake wa Marais Afrika, jijini Dar es Salaam jana. Mizinga alikuwa mmoja wa watoa mada katika mkutano huo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 03, 2013

    Du hata bush nae anakula konooooz

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 03, 2013

    hata joji bushi anakula KONOZ

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 04, 2013

    Naona Joji Bushi atakuwa mdau mkubwa wa globu ya jamii maana anakula konoz kama wadau wengine wa globu hii maarufu kona zote za ulimwengu.

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 04, 2013

    Huyu Bwana kweli ametupiga jeki kubwa sana katika kupambana na malaria na ukimwi. Tumshukuru sana kwa kuzingatia maslahi yetu pia! Karibu sana Joji!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...