Mkuu wa Jeshi la Magereza nchini, Kamishna Jenerali John Minja akimkaribisha Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dk Rehema Nchimbi (kushoto) katika hafla maalumu ya makabidhiano ya mizinga ya nyuki 85 iliyotengenezwa na jeshi hilo ambayo itatumika kufugia nyuki katika Mkoa wa Dodoma. Hafla hiyo imefanyika katika Viwanja vya Gereza Kuu Isanga, mjini Dodoma.
Mkuu wa Jeshi la Magereza nchini, Kamishna Jenerali John Minja akitoa hotuba fupi ya kumkaribisha mgeni rasmi, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dk Rehema Nchimbi kabla ya makabidhiano ya mizinga ya nyuki 85 iliyotengenezwa na jeshi la Magereza ambayo itatumika kufugia nyuki katika Mkoa wa Dodoma. Makabidhiano hayo yalifanyika katika viwanja vya Gereza Kuu Isanga, mjini Dodoma.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dk Rehema Nchimbi akitoa hotuba kwa maafisa wa Jeshi la Magereza kabla ya makabidhiano ya mizinga ya nyuki 85 iliyotengenezwa na jeshi hilo. Katika hotuba ake hiyo, Dk Nchimbi alimshukuru Mkuu wa Jeshi hilo nchini. Kamishna Jenerali John Minja kwa msaada huo mkubwa ambao utawahamasisha wakazi wa Mkoa wa Dodoma waweze kufuga nyuki. Makabidhiano hayo yalifanyika katika viwanja vya Gereza Kuu Isanga, mjini Dodoma. (Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.).

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 04, 2013

    Mbona hamna hizyo picha ya mizinga yeneyewe tuione?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...