Askari mgambo wakiwa katika eneo la kifunika mlima Kilimanjaro
wakiandaa chakula kwa ajili ya watu waliojitokeza kuzima moto katika
eneo hilo.
Kundi la asakari mgambo lililopo katika eneo la Kifunika mara baada ya
kufanikisha kuzima moto katika eneo hilo.

Sehemu ya eneo lililo athirika na moto mkubwa katika mlima Kilimanjaro.
Maeneo yaliyo athirika na moto mlima kilimanjaro.
Mwakilishi wa globu ya jamii akizungumza na mmoja wa wapagazi katika
mlima Kilimanjaro Mathayo Kunkwa kuhusiana na tukio la moto uliozuka
mlimani hapo.
Picha na habari na Dixon Busagaga
wa Globu ya Jamii, Moshi
wa Globu ya Jamii, Moshi
JUHUDI za makundi mbalimbali yaliyokuwa yakishiriki katika zoezi la
moto uliozuka mapema mwishoni mwa wiki iliyopita na kuteketeza zaidi
ya ekari 40 katika hifadhi ya mlima Kilimanjaro zimefanikiwa baada ya
kuudhibiti moto huo sasa kwa asilimia 99%.
Hadi kufikia Juzi makundi hayo wakiwemo askari kutoka chuo cha
taaluma ya Polisi cha Moshi (MPA),askari Mgambo kutoka wilaya za Rombo
,Moshi vijijini,Mwanga na Same wakiwemo maafisa kutoka hifadhi ya
mlima Kilimanjaro (KINAPA) walikuwa wamefanikiwa kuzima moto huo huku
kukiwa kumebakia na eneo dogo katika sehemu ya Kifunika.
Kwa takribani siku tano sasa eneo la mlima huo mrefu barani Afrika
lilikuwa likiteketea kwa moto huku chanzo chake kikidaiwa kuwa ni
shughuli za urinaji haramu wa asali uliokuwa ukifanywa na baadhi ya
wananchi katika hifadhi hiyo.
Mhifadhi mkuu wa hifadhi ya taifa ya mlima Kilimanjaro (KINAPA)Erastus
Lufunguro katika taarifa yake kwa mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Leonidas
Gama alisema hifadhi ya mlima huo inaendeleza doria kudhibiti visiki
vinavyotoa moshi ili usiwake tena.
Aidha mhifadhi Lufunguro alirejea kauli yake kwamba tukio la moto huo
ulioteketeza zaidi ya Hekari 40 katika hifadhi yam lima
huo,haujaathiri shughuli za
watalii kupanda na kushuka katika mlima huo wenye urefu wa Futi 5895
kutoka usawa wa Bahari.
alisema pamoja na kuzimwa kwa moto huo,bado kambi za watu zaidi ya 400
zilizoundwa katika wilaya za Rombo na Moshi kuukabili moto
huo,zinaendelea kukagua maeneo yote yaliyokuwa na moto na sasa
yanafuka moshi ili kuudhibiti usianze upya.
“Kinachofanyika sasa ni doria za mara kwa mara katika maeneo yote
ambayo moto ulikuwa ukiwaka ili kudhibiti iwapo utawaka tena kutokana
na upepo mkali katika eneo hilo lililotawaliwa na vichaka na misitu
mifupi”alisema Lufunguro.
“Baada ya moto kuripotiwa kuanza katika maeneo ya Amboni, Ushiri,
Keryo, Kimori na Shimbi wilayani Rombo mnamo Julai 7, tuliunda kambi
tano za Kilema, kifunika, Keryo, Maundi na Ujasiri zenye watu 467
ambao wamefanya kazi kubwa kuuzima moto” aliongeza Lufunguro .
Alisema pamoja na kambi za kuzima moto lakini pia hifadhi hiyo imeweka
kambi mbili maalum kwa ajili ya kuhudumia wanaoshiriki zoezi la kuzima
moto, ambapo moja ipo eneo la Nanjara wilayani Rombo ambapo ilikuwa na
sehemu kubwa ya moto.
Lufunguro alisema kambi nyingine ipo katka eneo la Marangu kwa ajili
ya kuhudumia eneo la Kilema juu ambapo zote kwa pamoja zilikuwa na
askari mgambo 128 kutoka wilaya zote za mkoa wa Kilimanjaro sanjari na
askari waliopo mafunzoni katika chuo cha polisi CCP.
Katika hatua nyingie mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Leonidas Gama akiwa
ameambatana na mkuu wa wilaya ya Moshi,Ibrahimu Msengi pamoja na
viongozi mbalimbali na kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa
walilazimika kupanda mlima Kilimanjaro hadi kituo cha Horombo kujionea
hali halisi ya athari iliyotokana na moto huo.
Moto Mlima Kilimanjaro,
ReplyDeleteYawezekana mojawapo ya haya hapa matatu (3),
1.JANGA ASILIA:
Linaweza kuwa ni janga asilia kwa kuwa maeneo yenye Milima au miinuko mikubwa Kijiografia inakuwa na ''internal bedrock dwindling as root cause to ingite fire or flames'' yaani mienendo ya miamba ya ndani kwa ndani ambayo hutoa misuguano na kuzalisha moto.
2.HUJUMA ZA MAJIRANI:
Pana wapinzani wetu wakubwa ktk Sekta ya Utalii nchi Jirani huko huko Kaskazini ya Tanzania ambapo hujuma inawezekana dhidi ya Mlima wa Kilimanjaro ambao ndio unaovuta Watalii wengi zaidi na kuifanya Tanzania kuibuka kidedea kwa Mapato ya Fedha za Kigeni.
3.HUJUMA ZA KISIASA:
Kama Siasa zetu nchini Tanzania zimeshakuwa na Taswira ya Ugaidi sio ajabuukakuta Mlima Kilimanjaro ukapigwa moto kwa sababu na Malengo ya Kisiasa.