![]() |
| Adam Sykes,Mrs Mganda,Ashura. |
Na Swahili TV Washington DC
Omar Sykes mwanafunzi raia wa Tanzania aliyeuwawa katika jiji la Washington, huenda akaenziwa kwa mtaa mmoja kupewa jina lake ili kuweka kumbukumbu na ujumbe kwa wote walioathirika na mauaji ya bunduki mitaani jijini Washington, Dc, na Marekani kwa ujumla. Kama pendekezo hilo litapitishwa atakuwa mtanzania wa kwanza kupewa mtaa nchini Marekani.
Akiongea katika shughuli ya kuuaga mwili wa marehemu Omar Sykes, meya wa jiji la Washington, mstahiki Vicent Gray, alisema kuwa anatarajia kupendekeza katika kikao kijacho cha halimashauri ya jiji mwezi Septemba kubadilisha mtaa wa Fairmont St, ambako mauti yalimkuta ili uitwe Omar Sykes Street.
Meya Gray aliongeza kusema kuwa kitendo hicho kitakuwa ni ujumbe kwa nchi nzima ya Marekani katika kuelezea ubaya wa ghasia za mauaji ya risasi mitaani. Marehemu Omar aliuwawa kwa risasi akiwa katika mazingira ya karibu na chuo kikuu anachosoma cha Howard.
Katika shughuli hiyo ya kuuaga mwiili , Swahili TV ilifanikiwa kuona baadhi ya viongozi maarufu waliohudhuria shughuli hiyo kama Naibu waziri wa mambo ya nje wa Marekani anayeshughulikia masuala ya Afrika Bi Jendayi Frazier alikuwa naibu waziri wakati wa utawala wa Bush 2005-2009.
Akiongea na Swahili TV, baba wa marehemu bwana Adam Sykes ambaye naye alikuwepo katika shughuli hiyo, alisema ni heshima ya pekee kwa taifa kubwa kama hili kumuenzi mwanae kwa kumpa jina la mtaa.
“Ni heshima ya aina gani kwa taifa kubwa kama hili kumuenzi mwanangu kwa kumpa mtaa”Alisema kwa majonzi huku akionesha furaha ya kupata heshima hiyo, bwana Sykes ambaye yeye na kaka Allyas Sykes waliwasili jumanne wiki hii nchini Marekani.
Swahili TV iliongea na wananchi mbalimbali waliohudhuria shughuli hiyo ambao wengi walionyesha hali ya majonzi ya kifo cha kijana huyo, mahojiano ya Swahili TV na baadhi ya viongozi wa serikali na Uongozi wa shule yatachapishwa na kuonyeshwa blog yetu.www.swahilitv.blogspot. com
Kwa picha za event ya Celebrating the life of Omar Sykes
BOFYA HAPA
Kwa picha za event ya Celebrating the life of Omar Sykes
BOFYA HAPA



MUNGU AMLAZE PEMA PEPONI NI HURUMA ..
ReplyDeleteILA SIJAELEWA INAONEKANA WENGI WAMEFURAHIA MTAA KUPEWA JINA BADALA YA KUANDAMANA MAUAJI YANAYOTOKEA U.S.A
UKITAZAMA MAUAJI KAMA HAYA SI MARA YA KWANZA KUTOKEA UKIACHILIA YA RAIA WENYEWE SIE TULIOPO MJE TUNAANGALIA TV CHANEL TLC NDO UTAONA HUKO KULIVYO
HATA WAWEKE JINA MAUAJI YA KAMA HAYO NI VIGUMU KUISHA WATU WANAMILIKI BUNDUKI ,VISASI NK
Pole sana mzee Sykes, mama, ndugu, jamaa na marafiki wote. Binafsi nadhani ni jambo jema kama utafanyika utaratibu wa kutafuta haki(justice). Kwa kuwa tunasikia nchi hiyo ni nchi ya haki, siyo? Ingawa tutakubaliana kuwa safari ya kudai haki ya kuuwawa kwa mtoto wako itakuwa ngumu na ndefu, lakini hatimae inaweza kupatikana. Ila inabidi serikali yetu iwe kama serikari za nchi zingine, yaani ikusaidie/ijisaidie! Na haki ikifanyika ni vema kwa upande wako kama mzazi na pia ni kinga kwa watu wengine walioko huko.
ReplyDeleteJina la mtaa waache waite, hata wakitaka kuita mji ni sawa tu. Maana jina ni jina, baada ya miaka kadhaa pia litaondolewa na kuwekwa jina jingine. Sisi tunacholilia ni haki, haki ndiyo itakayotulinda kwa kutuletea AMANI. Amani itatupa maisha marefu.
Watu wengi huamua kudai haki kwa kuwa ni jambo zuri au jema. Achilia mbali matokeo yake: Mtu apatapo haki yaku hufurahi, na hata kama haikupatikana bado kuna sehemu ya furaha kwa sababu alijaribu/ ulijaribu kudai.Kama haki isipopatikana basi fimbo ya myonge hulipwa na Mwenyezi Mungu
Kwa vipi mpaka sasa hatujaambiwa ni nini hasa, je alikuwa na maadui au ni bahati mbaya au ni vipi hasa!?
Fikilia kama ingekuwa ni mtu wao amefanyiwa hivyo hapa kwetu. Yamkini nchi nzima sasa hivi wote tungekuwa tunaruka kichura chura, toka Mkulu mpaka Chinga.
Namaliza kwa kusema tena pole na Mungu amlaze Marehemu mahala pema peponi- Amina
Poleni sana wafiwa wote, zaidi na zaidi mwazazi wa marehemu Omar Sykes. Allah awape subira kubwa sana na kumuombea dua mtoto wenu kwa huko aendako kwa muumba apate jazaa njema na kuwa miongoni mwa waja wema amin.
ReplyDeleteKumbukumbu ya maremu Omar Sykes ni jambo zuri ila isiifanye familia kukosa haki yake juu ya mtoto wenu. kazeni kamba kwa kudai haki itendeke mpaka mwisho wenu na Allah atasidia in sha allah.
Wote tunafahamu machungu ya kuondokewa ni makubwa sana kwenu kwani nyota mlioitegemea kuangaza baadae imezimika hafla kung'aa, lakini Allah ndie mjuzi wa yote na kila kitu.
Inah lilah waina ilayhi rajium.
Ujumbe mzuri kabisa.
ReplyDeletePoleni wafiwa
Poleni wafiwa. Pia jaribuni kutafuta mwanasheria atakaye fungua kesi ya kulipwa gharama za kuuwawa mtoto wenu. Hizi nchi za ughaibuni kama wangalijua kuruga basi ingekuwa hatari kuliko Afrika maana choyo na visasi ni vingi.
ReplyDeleteInna Lillah wa Inna Ilayhyi Rajiuuun!
ReplyDeleteTo ADAM, "Inna Lillah wa Inna Illahi Rajeoon," Adam pole sana sana, I know what you are going thru, because I also went thru of what you are, so I know how it feels, Inshaalah ALLAH atakupa SUBRA that is not a punishment but a trial, inshaalah utashinda To MDAU No.One "Ada ya mja kunena Muungwana ni Vitendo," shika bango uanze kuandamana kina sie tutajump into the wagon, It is easier say than done, Omar rest in peace justice will be done Inshaalah, without MAANDAMANO.
ReplyDelete