Waziri wa Fedha, , Dk. William Mgimwa amenukuliwa kwenye magazeti ya HNIPASHE na HabariLeo matoleo ya leo akisema kuwa Serikali sasa imekubali kuwa kodi mpya ya laini ya simu ni mgogoro na hivyo inakusudia kurejesha muswada wa sheria ulioazisha kodi hiyo wenye mkutano wa Bunge mwishoni mwa mwezi wa Agosti kwa mjadala zaidi na ufumbuzi kutoka kwa Wabunge.
Wiki iliyopita Rais Jakaya Kikwete alikutana na Wizara hiyo, Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia na wajumbe wa MOAT (Chama cha Wamiliki wa Kampuni za Simu - TTCL, Airtel, Vodacom, Tigo na Zantel) Ikulu kusikia pamoja na mambo mengine, kuondolewa kwa kodi ya simu kutakavyokwaza maendeleao ya sekta ya mawasiliano na kuwataka MOAT kutoa mapendekezo ya jinsi serikali itapata kiasi cha Sh. bilioni 178 zilizopangwa kupatikana katika bajeti ya serikali ya mwaka wa fedha wa 2013/14 kutokana na kodi ya simu.
Kodi hizo za Shilingi 1,000 kwa mwezi ambazo Waziri Dk Mgimwa akiwasilisha makaridio ya mapato na matumzi kwa Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2013/14 Bungeni mwezi Juni tarehe 13, mwaka hu, alisema:
- Zilianza kutozwa na serikali mwanzoni mwa Julai, mwaka huu hivyo kuwalazimu wamiliki wa simu nchini kuingia gharama zaidi kwa asilimia 14.5 ili kuongeza mapato.
- Serikali inakusudia kutoza ushuru kwenye huduma zote za simu za mkononi, kama chanzo kipya cha mapato ya badala ya muda wa maongezi peke yake.
- Asilimia 2.5 ya mapato ya kodi hiyo yatatumika kugharimia elimu nchini kwa kuzingatia mapendekezo ya Kamati Maalumu ya Spika ya Kushauri kuhusu mapato na matumizi ya Serikali.
- Inaanzishwa kodi ya zuio ya asilimia 10 ya kamisheni ya usafirishaji wa fedha kwa njia ya simu za mkononi ambazo zitakusanywa na kampuni za simu kutoka kwa Wakala wanaotoa huduma hizo kupitia simu za mkononi.
- Mapendekezo hayo ni utekelezaji wa ushauri wa Mdhibiti na Mkaguzi wa Hesabu za Serikali (CAG), Ludovick Utouh kuwa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), itafute vyanzo vipya vya kodi ili kuongeza mapato ya Serikali.


Kwanini serikali isitafute fedha hizi ktk makampuni ya madini badala ya kuwakamua hadi walalahoi?
ReplyDeleteMbona ktk bajeti sikusikia kuongeza ushuru ktk makampuni ya madini? nini 'kimejificha' nyuma ya pazia?
Nashauri bunge isifute kodi hii kwa mustakabali wa maendeleo nchini! Makelele ya wanasiasa wanaochochea hili yasiyumbishe serikali, huku mtaani kiukweli wengi hawapigi makelele kama inavyochochewa. Chonde chonde wabunge na serikali tunahitaji maendeleo na si malumbano ya kuturudisha nyuma.
ReplyDeleteWe unayesema wabunge waache kuchochea wananchi ndo hufai, unauelewa wowote kuhusu uchumi au kodi wewe, sasa hivi tozo zimeongeka kwenye huduma za simu hadi zinazidi mabenki isipokuwa stanbic (wakoloni) kila unachotumia unakilipia kodi zaidi ya tatu au nne,kwa hiyo usiwalaumu wabunge, kadi ya mishahara wamepunguza 1% hiyo imesaidia nini kwa mtanzania, kwa nini usishauri serikali iangalie kodi za nyumba tuzolipa wamiliki kwani tunalipa hela nyingi kama ziara ya wakuu wa nchi za africa waliokuja hapa tz kwenye mkutano, imebainika kuna upotevu wa bilion karibia mbili baada ya watu kufeki kampuni kwa ajili ya kutoa huduma, vinywaji, chakula n.k. Hivi hizo sio kodi? watanzania ifike mahali tuheshimu mamlaka na kuwa na hofu ya MUNGU kwa tamaa. Migodi yenyewe inamilikiwa na wabunge, yaani tanzania hatuandai mazingira mazuri ya huduma muhimu na maendeleo ya kiuchumi kwa ajili ya vizazi vijavyo bali tunaandaa taifa tegemezi la wavivu wa kujituma na kuibia wengine.
ReplyDeleteKucha mbayaaaa!
ReplyDelete