Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais, Mheshimiwa Charles Kitwanga akikagua mfumo wa maji taka katika kiwanda cha 21st Century Textile Mill mkoani Morogoro
 Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais, Mheshimiwa Charles Kitwanga akiangalia sehemu ya kuni/magogo yaliyokusanywa na kiwanda cha 21st Century Textile Mill mkoani Morogoro. Wengine ni Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Bw. Joel Bendera na Mkuu wa Wilaya Morogoro Bw. Said Amanzi
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais, Mheshimiwa Charles Kitwanga (kulia) akitoa maelezo ya kiutendaji kwa Bw. P.V.Singh, Afisa Mtendaji Mkuu wa Kiwanda cha  Century Textile Mill mkoani Morogoro juu ya uharibifu mkubwa wa mazingira unaotokana na nishati ya kuni/magogo yanayotumiwa kiwandani hapo katika shughuli za uzalishaji. Katikati ni Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Bw. Joel Bendera na Mkururenzi Mkuu wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) Eng. Bonaventure Baya

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 09, 2013

    Huyu atatembelewa mara ngapi na viongozi na kwa madhumuni gani??? Kwa nini kiwanda hakifungwi na mhusika kuchukuliwa hatua za kisheria? Kuna nini hapa!!

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 09, 2013

    Mm sikusoma lakini kwa macho yangu ma3 najua fika kabisa hiki kiwanda kinaharibu misitu yetu nakuombeni mkifunge haraka sana,,mkuu wa mkoa wafanyann? Tuachieni moro yetu iwe kijani na fukuzeni wahindi wooote hapo moro coz hawana faida kwetu.

    ReplyDelete
  3. Ni aibu kwa taifa,kwa wataalamu,ofisi ya Makamu wa Rasi mazingira,Kwa wizara husika na kwa vijana wa Tanzania Kuwa na kiwanda cha kuni eti wawekezaji katika karne hii ya 21.
    Ushahidi upo kuwa kiwanda hicho kimemaliza miti mkoani Morogoro na hasa maeneo ya Kiperi na Mlali na pengine kwingineko-ukiwaona viongozi wa vijiji na baadhi ya wancnhi wanajua sana.Huku kusema kuwa wananunua miti toka Iringa hizo ni mbwembwe tu,kama wananunua basi ni sample.Naomba Wataalumu wafike wahoji na kufanya utafiti wanatumia magogo kiasi ganikwa siku kwa mwezi na waangalie aina ya miti hapo kwa kuchukua samples na kuzikagua vizuri,watagundua waliyonunua toka mashamba halali ya miti ni kiasi gani.Kama kuna watu wana linda kiwanda hicho basi kuna Rushwa kubwa au mkono wa Fisadi mmoja serikalini anayewalinda na ananufaika na kiwanda hicho.
    KIWANDA HICHO NI HATARI ZAIDI YA UKIMWI NA MALALIA,NI HATARI ZAIDI YA VIRUSI.
    Na kama uwekezejai ndio huo basi Tanzania imekwisha.Je wamepanda hekta ngapi za miti toka waje?Je wamefadhili uzalishaji wa miti na upandaji wa miti kwa kiasi gani?
    Je serikali inapata faida kiasi gani iliyosambamba na hasara kwa taifa??AMKA,FUATILIA,WAJIBIKA.

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 09, 2013

    Nishati mbadala ipo? Makaa ya mawe? Gesi? n.k. Manake tusije tukawa tunasema kifungwe na huku hatujui nishati mbadala ni nini?

    Lengo hasa ni matumizi ya kwenye BOILERS??? Gesi haijafika hapo Morogoro? Na umeme ni wa mtihani? Viwanda tunahitajika kwa ajili ya ku-process pamba yetu na kuwa na nyuzi za nguo na hatimaye nyuzi kamili.

    Hapa inabidi serikali ibanwe ipeleke nishati mbadala Morogoro mzima halafu ndiyo waanze kuchukua hatua kwa viwanda visivyotumia nishati mbadala. Kwa sasa si rahisi, unless tuwe tunazungumza siasa; kama inavyotugharimu sakata la DOWAS, ambapo tukaacha kununua mitambo tukaleta siasa. Sasa sijui tumeruka nini??? Tunalipa umeme unaozaliswa na SYMBION!!! Kazi kweli kweli, tutumie ubongo Watanzania, tusichukulie kila kitu juujuu sana na kisiasa siasa tu.

    Marekani bado hawajaamua kufunga moja kwa moja matumizi ya Refrigerants kama R22, R12, ... Wanasema bado wanaendelea kutafuta mbadala, ndiyo maana hawaja-sign Kyoto protocol. Yani kwa ujumla hawakurupuki, wanatathmini, FULL SIMULATION

    ReplyDelete
  5. AnonymousJuly 09, 2013

    kiwanda kifungwe mpaka watakapopata nishati mbadala ambayo ni rafiki kwa mazingira ndipo waruhusiwe kuendelea na shughuli zao.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...