Naibu
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la
Taifa la Usalama Barabarani, Pereira Ame Silima (kulia) akimkabidhi tunzo Rais
wa Chama cha Wadau wa Magari (AAT), Nizar Jivani kwa ajili ya chama chake
kutoa mchango mkubwa kwa kutoa mafunzo ya uendeshaji kwa madereva 2500 wa
pikpiki, ambao tayari wamehitimu mafunzo hayo yaliyotolewa jijini Dar es
Salaam kuanzia Julai 2012 hadi Julai 2013. Makabidhiano hayo yalifanyika
Makao Makuu ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi leo. Kulia ni Kamanda wa
Kikosi cha Usalama Barabarani, Mohammed Mpinga.
Naibu
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la
Taifa la Usalama Barabarani, Pereira Ame Silima (kulia) akiwafafanulia
waandishi wa habari, jisni Chama cha Wadau wa Magari nchini (AAT),
kilivyokuwa kinatoa mchango wake kwa kutoa mafunzo ya uendeshaji pikpiki
kwa jina maarufu bodaboda. Madereva 2500 wa pikpiki walihitimu mafunzo
hayo yaliyotolewa jijini Dar es Salaam kuanzia Julai 2012 hadi Julai 2013.
Naibu
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la
Taifa la Usalama Barabarani, Pereira Ame Silima (wapili kutoka kulia)
akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Chama cha Wadau wa Magari
(AAT) Nizar Jivani na Yusuf Ghor. Kulia ni Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Mohammed Mpinga. Naibu Waziri Pereira alitoa tunzo kwa
uongozi wa AAT kwa ajili ya kutoa
mafunzo ya uendeshaji pikpiki kwa jina maarufu bodaboda. Madereva 2500 wa
pikpiki walihitimu mafunzo hayo yaliyotolewa jijini Dar es Salaam kuanzia
Julai 2012 hadi Julai 2013. Picha
zote na Felix Mwagara, Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali, Wizara ya
Mambo ya Ndani ya Nchi.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...