NMB kwa kupitia idara yake ya biashara za Kilimo (Agribusiness Department) leo imetoa ripoti mbili;
1. Utafiti wa kujua kama mfumo wa stakabadhi mazao ghalani (Warehouse Receipt Financing Sytem) una manufaa kwa wakulima au la? Utafiti umethibitisha kuwa mfumo una manufaa kwa wakulima japokuwa kuna changamoto bado. Mfano wakulima wa kahawa wanaouza mazao yao kupitia mfumo wa stakabadhi ghalani wanapata zaidi ya asilimia 30% ukilinganisha na wale wasiotumia mfumo wa stakabadhi ghalani.
2. Utafiti wa sekta ya sukari unaonesha kuwa Tanzania inatumia wastani wa tani 520,000 kwa mwaka (ikiwemo sukari kwa matumizi ya viwanda) kati ya hizo uzalishaji ni tani 300,000 na kiasi cha tani 220,000 zinaingizwa kutoka nje kwa mwaka. Utafiti umeonesha kwamba Tanzania inaweza kuzalisha kiwango cha kutosheleza mahitaji ya nchi iwapo kutakuwa na kilimo cha umwagiliaji, miche bora ya miwa, pembejeo za kilimo zilizo bora ikiwemo mbolea pamoja na mazingira bora ya uwezeshaji (enabling environment) wa sekta ya sukari.
 |
Maofisa wa NMB Idara ya biashara ya Kilimo, kwanza kulia ni Sierk Plaat ambae ni Mchambuzi Mwandamizi toka benki ya Rabobank, Robert Paschal Mkuu wa Idara Mikopo ya Kilimo NMB na Carol Nyangaro Mtafiti, Mchambuzi wa mambo ya kilimo wakionyesha kitabu ambacho kimebeba ripoti ya mfumo wa stakabadhi ghalani |

Mkuu wa Idara ya biashara za kilimo NMB, Robert Paschal (kati) akiongea na waandishi wa habari na kuwasilisha ripoti ya biashara za kilimo zifanywazo na Benki ya NMB
Sehemu ya waandishi wa habari waliohudhuria hafla ya uwasilishaji wa ripoti ya biashara ya kilimo
Sehemu ya maofisa wa NMB wanaoshiriki Maonesho ya Biashara yanayoendelea
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...