Rais Jakaya Mrisho Kikwete akijibu maswali toka kwa wanahabari wakati wa mkutano wa pamoja na waandishi wa habari mara baada ya mkutano wa siku moja wa Kamati ya Troika ya Siasa na Usalama ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC Organ Troika on Politics, Defence and Security Cooperation) katika jumba la wageni wa Rais la Sefako Makgatho jijini Pretoria, Afrika Kusini, Jumamosi usiku. Kutoka kulia ni Rais wa Afrika Kusini Mhe Jacob Zuma, Rais wa Msumbiji ambaye pia ni mwenyekiti wa SADC Mhe Armando Guebuza, Katibu Mtendajji wa SADC Dkt Tomaz Augusto Salomão na Waziri wa Mambo ya Nje wa Namibia Netumbo Nandi-Ndaitwah.
Ujumbe wa Tanzania katika mkutano wa siku moja wa Kamati ya Troika ya Siasa na Usalama ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC Organ Troika on Politics, Defence and Security Cooperation) katika jumba la wageni wa Rais la Sefako Makgatho jijini Pretoria, Afrika Kusini, Jumamosi usiku.
Mwenyekiti wa Kamati ya Troika ya Siasa na Usalama ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC Organ Troika on Politics, Defence and Security Cooperation), Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongozana na Rais Jacob Zuma wa Afrika Kusini na Rais Armando Guebuza baada ya mkutano wa kamati ya Troika katika jumba la wageni wa Rais la Sefako Makgatho jijini Pretoria, Afrika Kusini, Jumamosi usiku.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza na viongozi wa Jumuiya za Watanzania waishio Afrika ya Kusini leo Julai 21, 2013 jijini Pretoria, Afrika ya Kusini, muda mfupi kabla ya kurejea nyumbani baada ya kuhudhuria mkutano wa siku moja wa Kamati ya Troika ya Siasa na Usalama ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC Organ Troika on Politics, Defence and Security Cooperation).

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 22, 2013

    ankali unaniachaga hoi unapotangulia kwenye msafara wa mkubwa ukifika hiyo nchi unaanza kwa kuweka picha au video eti upo kwenye vekesheni hahahaha

    leo umetuwekea video upo maeneo ya hospital alipolazwa madiba na sasa unatuonyesha picha za mkubwa akiwa huko kwa madiba

    safi sana napenda unavyotumia nafasi ya safari hizo kutuonyesha mambo mbali mbali na kutufungua macho

    mungu akuzidishie ankali umenisaidia kwa kiasi kikubwa kupata mambo mengi yanayojili huko nyumbani

    pole kwa kazi na swaum.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...