Mgeni
rasmi, Rais Jakaya Kikwete akizindua huduma mpya ya Benki ya Posta iitwayo TPB
POPOTE mapema leo mchana kwenye hotel ya Serena jijini Dar ,hafla hiyo
imewakutanisha wadau mbalimbali wa mambo ya kibenki na wengineo, lengo kuu ya uzinduzi
wa huduma hiyo ikiwa ni kuweka na kutoa
fedha kupitia Mawakala wa Benki ya Posta nchini Tanzania.Kushoto ni
Waziri wa Fedha Dkt.William Mgimwa, Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya Posta,Profesa
Lettice Rutashobya na kulia kwake ni Afisa Mtendaji Mkuu wa benki hiyo
Bw.Moshingi wakishuhudia tukio hilo adhimu kabisa.
Rais Jakaya Kikwete akijaza fomu yake ya huduma hiyo mpya ya TPB POPOTE iliyozinduliwa na Benki ya Posta mapema leo mchana kwenye hotel ya Serena jijini Dar ,hafla hiyo imewakutanisha wadau mbalimbali wa mambo ya kibenki na wengineo, lengo kuu ya uzinduzi wa huduma hiyo ikiwa ni kuweka na kutoa fedha kupitia Mawakala wa Benki ya Posta nchini Tanzania.Pichani kulia ni Waziri wa Fedha Dkt.William Mgimwa, Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya Posta,Profesa Lettice Rutashobya na kushto ni Afisa Mtendaji Mkuu wa benki hiyo Bw.Moshingi wakishuhudia tukio hilo adhimu kabisa.
Rais Kikwete akipewa maelezo mafupi namna ya kuitumia huduma hiyo ya TPB POPOTE kutoka kwa mmoja wa wafanyakazi wa Benki ya Posta.
Rais Jakaya Kikwete akikabidhiwa kadi yake mpya ya huduma mpya TPB POPOTE na Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Posta Bw.Moshingi ,mara baada ya huduma hiyo kuzinduliwa rasmi mapema leo .
Mgeni rasmi,Rais Kikwete akikabidhiwa zawadi kut0ka kwa Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya Posta,Profesa Lettice Rutashobya .
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...