https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhzRgyOe7RjsHo3ihmpexX7YqEyvEolnou9VYnQ6uvVxR2Kntu01QCNvY2V_u0H9TQZNJDLUTuFMEUBCM9DPu4rc9slQqjt87EZX7uUhcX15w_7633LzuPohAQreEiordxQgzmYXA/s640/DSC_0430.JPG
 Hivi ndivyo hali halisi huwa wakati wa maska barabara ya Tunduru

Na Steven Augustino, Tunduru
SERIKALi imewataka wakazi wa Wilaya ya Tunduru Mkoani Ruvuma kuondoa mashaka juu ya ujenzi wa Miundombinu ya Barabara ya Lami ambayo ilisimama kwa zaidi ya miezi sita ikidai kuwa ujenzi wake utaanza mwanzoni mwa mwezi Oktoba mwaka huu.

Kauli hiyo ya matumaini kwa Wananchi hao ilitolewa na Waziri Mkuu wa Jamuhuri ya muungano wa Tanzania Mizengo pinda wakati akiongea na wananchi wa Kijiji cha Milonde katika Ukumbi wa AULA uliopo katika taasisi ya KIUMA Wilayani humo.

Akifafanua taarifa hiyo alisema kuwa Barabara hiyo ambayo ilikuwa chini ya mkandarasi, Kampuni ya Progresvu Co LTD Serikali ilishindwa kuendelea na mkataba wa ujenzi wake baada ya kubaini kuwa ilidanganywa na mkandarasi huyo kwa madai kuwa anao uwezo lakini hali halisi akiwa hana uwezo wa kukamirisha barabara hiyo kwa wakati.

Alisema pamoja na mambo mengine hivi sasa serikali inakubaliana na ombi la wananchi wa Wilaya hiyo la kuitaka Serikali iiangalie Wilaya ya Tunduru kwa Jicho la huruma ili kuwakwamua wananchi wake ambao uchumi wao umekaliwa na kutofunguka kwa miundombinu hiyo ya barabara.

“Tulikatisha mkataba na kampuni hiyo baada ya kubaini kuwa mkandarasi huyo aliidanganya Serikali yetu" alisema Pinda na kuongeza kuwa kwavile fedha za ujenzi wa mradi huo wa kilometa 1992 zipo serikali imejipanga upya na kuhakikisha kuwa mradi huo unakamilika kwa wakati ili kuwaondolea wananchi adha ambayo wamekuwa wakiipata kwa muda mrefu.

Awali akisoma taarifa ya taasisi hiyo Mkurugenzi wa KIUMA Dkt. Matomora Matomora alimweleza waziri Mkuu kuwa kitendo cha kutofunguliwa kwa barabara za Tunduru / Namtumbo na Tunduru/ Mangaka kunaonekana kuwa ni kikwazo kikubwakinacho watia umasikini wananchi wanaoishio katika Wilaya hizo zilizopo maeneo ya kusini kati.

 Dkt. Matomora aliendelea kueleza kuwa kutoka na kutofunguka kwa barabara hizo Wilaya zote za Kusini kati zimekuwa zikiachwa nyuma na Wilaya zilizofunguka katika maendeleo ya Elimu,afya na kilimo ambavyo ili huduma zake ziweze kukamilika zinahitaji wataalamu na vifaa kutoka katika maeneo mengine ya nchi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 16, 2013

    Dereva hajui kutumia "4 wheels gear" na kusababisha Mheshimiwa kuingia matope bure!!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...