Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein,(katikati) akijumuika na Vingozi na Waislamu wengine katika Hitma ya wanajeshi waliouwawa kwa kupigwa risasi Jimbo la Daafur nchini Sudan hivi karibuni,Merehemu Sgt Shaibu Shehe Othman, na Cpl Mohammed Juma Ally iliyosomwa katika msikiti Masjid Nuru Muhammad,Mombasa Mjini Unguja leo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein,(wa tatu kulia) akijumuika na Vingozi na Waislamu wengine katika kuwaswalia Merehemu Sgt Shaibu Shehe Othman,na Cpl Mohammed Juma Ally ,mbele katika msikiti Masjid Nuru Muhammad,Mombasa Mjini Unguja leo,wanajeshi waliouwawa kwa kupigwa risasi Jimbo la Daafur nchini Sudan hivi karibuni.
Wanajeshi wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania wakibeba Jeneza la mwili wa Marehemu Sgt Shaibu Shehe Othman,baada ya kuwasilim katika makaburi ya Mwanakwerekwe mjini Zanzibar jana,akiwa ni miongoni mwa wanajeshi 7 waliouwawa kwa kupigwa risasi Jimbo la Daafur nchini Sudan hivi karibuni.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein,(wa pili kushoto) na viongozi wengine walihudhuria katika mazishi ya Marehemu Sgt Shaibu Shehe Othman, katika makaburi ya Mwanakwerekwe mjini Zanzibar jana,akiwa ni miongoni mwa wanajeshi 7 waliouwawa kwa kupigwa risasi Jimbo la Daafur nchini Sudan hivi karibuni.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein,akitia udungo katika Kaburi la Marehemu Sgt Shaibu Shehe Othman,aliyezikwa leo Mwanakwerekwe Mjini Unguja, akiwa ni miongoni mwa wanajeshi wa jeshi la Ulinzi la Tanzania 7 waliouwawa hivi karibuni Nchini Sudan Jimbo la Daafur.
Baadhi ya Wanajeshi wa Jeshi la Ulinzi la Tanzania na Ndugu na Jamaa wa marehemu Sgt Shaibu Shehe Othman, na Cpl Mohammed Juma Ally ,waliofurika katika viwanja vya makaburi ya Mwanakwerekwe,ambapo ndipo walipozikwa leo,mchana.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein,(katikati) na Vingozi na Waislamu,wakiangalia Wanajeshi wa Jeshi la Ulinzi la Tanzania,walipokuwa wakitoa hesha ya mwisho kwa marehemu Sgt Shaibu Shehe Othman,wakati wa mazishi yake katika makaburi ya Mwanakwerekwe leo.Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 23, 2013


    Inna Lillahi wa inna ilayhi Raji un

    Truly, to Allah we belong and truly, to Him we shall return.
    [Noble Quran 2:156]

    ReplyDelete
  2. INNA LILLAH WAINNA ILAYHI RAJIUN. Mwenyez Mungu wapokee waja wako na uwaghufirie kwa yote, uwapumzishe katika kivuli chako na kesho Yaumul-Hisabu, uwaingize katika FIR'DAUS yako wabakie humo daima dawamu - AMEEN.

    Halafu huyo mwenye kamera hapo pichani, yaani hana hata woga, maana anataka akhitimishe mpaka kilichopo kwenye mwanandani. Nadhani tuwe na kiasi jamani tusianze kufurutu ada, tuzingatie taratibu za mazishi katika Imani yetu zina mipaka gani.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...