Na. James Katubuka
Serikali
kupitia Ofisi ya Rais,Menejimenti ya Utumishi wa Umma imesaini mkataba kwa ajili ya kuunda mfumo wa kutoa huduma za
kitabibu kwa njia ya elektroniki ili kuwawezesha wananchi kupata huduma bora kwa
wakati.
Akisaini
mkataba huo leo,Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais,Menejimenti ya Utumishi wa Umma Bw.
George D. Yambesi alisema mkataba huo utawezesha kuboresha huduma katika sekta
ya afya nchini. “Mfumo
huu unatarajiwa kuleta mabadiliko makubwa katika huduma za kitabibu zitolewazo
na Sekta ya Afya” alifafanua Bw. Yambesi.
Naye,
Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili Dkt. Marina Njelekela
alisema, kupitia mfumo huu huduma za kitabibu zinaweza kutolewa na Daktari Bingwa
aliyepo Muhimbili kwa wagonjwa walio katika hospitali zilizo katika maeneo
mengine bila ya wagonjwa hao kupewa rufaa ya kuja kupata huduma hiyo Muhimbili.
“Mfumo
huu utawawezesha madaktari kubadilishana ujuzi wa kitabibu kwa urahisi zaidi
hivyo kuboresha huduma za afya nchini” alifafanua Dkt. Njelekela.
Akizungumza
kwa niaba ya Kampuni ya kutoa ushauri elekezi, Meneja Mradi wa Swiss
Tropical and Public Health Institute Bw. Reinhold Werlein aliitaka Serikali
kutoa ushirikiano ili kufanikisha matumizi ya mfumo huo.“Mshauri
mwelekelezi pekee hawezi kuuwezesha mfumo huu kufanya kazi kwa ufanisi hivyo
ametoa wito kwa Serikali kutoa ushirikiano wa kutosha ili mfumo huu uweze kuwa
na manufaa kwa watanzania” alisisitiza Bw. Werlein.
Uwepo
wa mkataba huu kwa ajili ya kuunda mfumo wa kutoa huduma za kitabibu kwa njia
ya electroniki ni mojawapo ya jitihada za Serikali katika kuboresha huduma
katika sekta ya afya nchini.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...