Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt Fenelle Mukangara kulia akizungumza na Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Standard Chartered Tanzania Bibi Liz Lloyd alipomtembelea ofisini kwake leo jijini Dar es Salaam. Katika mazungumzo yao walijikita katika kuangalia namna ambavyo benki ya Standard Charterd Tanzania inaweza kushirikiana na Serikali kuwawezesha Vijana kukabiliana na changamoto za maisha.
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt Fenelle Mukangara kulia akiagana na Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Standard Chartered Tanzania Bibi Liz Lloyd alipomtembelea afisini kwake leo jijini Dar es Salaam kuzungumzia kuhusu benki uwezeshaji wa Vijana kupitia Standard Chartered Bank Tanzania Limited.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...