Mkurugenzi wa mamlaka ya maji safi na maji taka mjini
Moshi (MUWSA) Cyprian Luhemeja akichangia jambo katika kikao cha naibu
waziri wa maji Dk Mahenge na watendaji wa idara ya maji.
Mbunge wa jimbo la Moshi vijijini Dk Cyril Chami akichangia jambo
katika kikao hicho.
Naibu waziri wa maji Dk Binilith Mahenge(aliyesimama) akizungumza na
watendaji wa maji pamoja na viongozi wa kamati ya ulinzi na usalama ya
mkoa katika ofisi ya mkuu wa wilaya ya Moshi.waliokaa kutoka shoto ni
Suleiman Moshi(RSO),Mkuu wa wilaya ya Moshi Dk Ibrahim Msengi na wa
mwisho kamanda wa polisi mkoa wa Kilimanjaro Robert Boaz.
Mhandisi wa maji wilaya ya Moshi vijijini Brown Lyimo akitoa maelezo
mbele ya naibu waziri wa maji Dk Mahenge alipotembelea mradi wa maji
wa Mbokomu wilaya ya Moshi vijijini.
Miongoni mwa mambo ambayo yalionekana kumkera naibu waziri ni pamoja
na upotevu huu wa maji kama inavyoonekana hapa huku wahusika wakiweka
mti ili kuzuia maji yasitoke badala ya koki.hapa naibu waziri
akimuuliza mhandisi wa iwlaya kuhusu tatizo hilo.
Na Dixon Busagaga wa globu ya jamii,Moshi
SERIKALI imetaka mamlaka za maji safi na usafi wa mazingira nchini
sanjari na halmashauri za miji,manispaa na majiji kuipa kipaumbele
miradi ya maji katika maeneo ili kupunguza uwezekano wa kuwapo kwa
maradhi ya milipuko yanayochangiwa na ukosefu wa maji safi na salama.
Naibu waziri wa maji Dk Bilinith Mahenge aliyasema hayo wakati
akizungumza na viongozi wa wilaya ya Moshi wakiwamo wakurugenzi wa
halmashauri za Manispaa ya Moshi na Moshi vijijini wakati wa ziara
yake ya siku sita mkoani Kilimanjaro kukagua utekelezaji wa miradi ya
maji.
Amesema kuna umuhimu kwa mamlaka na miji hiyo kutenga sehemu ya fedha
katika bajeti zao kila mwaka kwa ajili ya utekelezaji wa mradi wa maji
huku wizara ikiendelea kutoa misaada katika miradi mikubwa na masuala
ya kiufundi.
“Lazima mtenge fedha za miradi ya maji kila mwaka,msipofanya hivyo,
sisi tunajua hilo siyo jambo la kipaumbele, lakini kumbukeni
upatikanaji wa maji unawasaidia wananchi kupunguza fedha ambazo
wangetumia kwa matibabu baada ya kuugua matumbo na watazifanyia
shughuli za kiuchumi”alisema.
Kuhusu wingi wa maji naibu waziri alipongeza juhudi za mamlaka ya maji
safi na usafi wa mazingira mjini Moshi(MUWSA) kwa kuvitunza vyanzo vya
maji Nsere, uchimbaji kisima cha eneo la longuo, tanki la kuhifadhi
maji Kilimanjaro na CCP ambavyo kuna miti yenye kuhifadhi maji.
Akizungumzia mradi wa vijiji 10 unaofadhiliwa na benki ya dunia,
alitaka kila halmashauri kuhakikisha unatekelezeka kwa wakati ili
kupunguza idadi ya watu wanaokosa maji.
Hata hivyo alikiri kuwapo kwa changamoto ya mgawo wa vijiji 10 hata
kwa halmashauri ambazo ni kubwa zenye vijiji zaidi ya 100 ambazo nazo
zinatakiwa kuainisha vijiji 10 jambo ambalo alidai linatakiwa
kutazamwa upya.
“Lazima tuangalie upya vigezo vya ugawaji wa mafungu ya fedha kwa
kuzingatia ukubwa wa wilaya kwani sasa inazingatia idadi ya watu,aina
ya teknolojia ya mradi wa maji,maeneo mengine teknolojia mtiririko
ambayo ni gharama sana na mengine ni ya visima au mabwawa”alisema.
jamani kweli ni mkoa kama kilimanjaro mpaka leo maji ni tabu majumbani hakuna na bomba na visima venyewe ni hewa vyanzo vya maji mmeviua hatari kweli serikali yetu bongo tambarare
ReplyDelete