Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Saidi Mwema akipokea zawadi ya mfano wa mashua kutoka kwa mwakilishi wa kikundi cha ulinzi shirikishi cha shehia ya Stone Town, Saidi Mkweche wakati wa sherehe za uzinduzi wa upanuzi wa zahanati ya Polisi, Ziwani Visiwani Zanzibar  jana. Picha na Hassan Mndeme-Jeshi la Polisi.
 Wanafunzi wa kikundi cha sanaa cha Shule ya Msingi Matopeni Unguja, wakiimba nyimbo ya kuhimiza vijana kuacha dawa za kulevya, baada ya IGP Saidi Mwema kufanya uzinduzi wa  upanuzi wa zahanati ya Polisi, Ziwani, Visiwani Zanzibar  jana. Picha na Hassan Mndeme-Jeshi la Polisi.
Hapsa Omar wa kikundi cha Kung Fu cha Shehia ya Nyerere akifanya onyesho la kung fu dhidi ya mpinzani wake Nassir Hassan jana Visiwani Zanzibar baada ya IGP Saidi Mwema kufanya  uzinduzi wa upanuzi wa zahanati ya Polisi, Ziwani Visiwani Zanzibar  jana. Picha na Hassan Mndeme-Jeshi la Polisi. Picha na Hassan Mndeme-Jeshi la Polisi

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 22, 2013

    Hahahahah!

    Hilo teke la 'Bandama' Picha ya chini ambalio Hapsa Omar alilomrushia Mpinzani wake Nasser Hassan si mchezo!

    Si dogo anaweza kuomba maji kwa kiu ndani ya Mfungo?

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 22, 2013

    IGP wachukulie hatua kali hao vijana wa kung-fu hapo maana si katiba inakataza vikundi vya ulinz vyenye mazoez ya kijeshi...lazima watakuwa red brigade watarajiwa hao afande!..ha ha

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 23, 2013

    Duhhh Dogo alivyorusha teke hewani ni kama Jet Li !

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...