Shilole (kati) akipata picha ya pamoja na Bwn. Idd Sandaly(kushoto) Rais wa Jumuiya ya Watanzania DMV na mjumbe wa kamati ya maandalizi ya sherehe ya miaka 3 ya Vijimambo na Tamasha la Utamaduni wa kiswahili Marekani litakalofanyika Jumamosi July 6, 2013 Capitol Heights, Maryland. Kulia ni mwenyekiti wa kamati hiyo ya maandalizi, Bwn. Baraka Daudi.
Katibu wa kamati ya maandalizi ya sherehe ya miaka 3 ya Vijimambo na Tamasha la Utamaduni wa Kiswahili Marekani, Bi. Asha Nyang'anyi katika picha ya pamoja na Shilole kwenye TAMCO famuly day iliyofanyika Jumapili June 30, 2013.
Halima Ali (kati) akipata picha ya pamoja na Masanja Mkandamizaji na Shilole.
Wadau wa DMV wakipata picha ya pamoja na Shilole na Masanja.
Muhtar akipata picha ya pamoja na Masanja. 
Mrs Haward katika picha ya pamoja na Masanja na Shilole.
Wadau katika picha ya pamoja na Shilole.
Mr & Mrs Sebo wakipata Ukodak moment na Shilole.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 15 mpaka sasa

  1. Kaka,

    Sasa huyo MASANJA kwa nini aliamua kuwatangaza WATANI WA JADI badala ya NCHI YAKE MWENYEWE jamani?
    Ni makusudi au alijisahau?

    Khaah!

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 01, 2013

    Huyo Masanja kwani ni Mkenya au Mtanzania? mbona kavaa T-shirt yenye nembo ya Kenya?

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 01, 2013

    Wabongo bwana ujinga umewatawala. Masanja yupo nje ya Tz anapaswa kuitangaza Tanzania lakini ona amevaa T-shirt ya Kenya. Ooooooovyo kabisa na uigizaji wake!

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 01, 2013

    MHHH! SASA WEWE MASANJA KUVAA T-SHIRT YA KENYA NDIYO NINI? OVYOOOOO000000!!

    ReplyDelete
  5. HUU KWELI NI UDHAIFU KWA WASANII WETU,YAAN DHUMUNI MOJA WAPO KUTOKA NJE YA NCHI NI KUTUWAKILISHA NA KULITANGAZA TAIFA LETU SASA IWEJE NAFUNGUA PICHA NAMUONA MSANII WETU WA KITANZANIA TENA KATIKA WALIYO JUU KATIKA FANI UA UIGIZAJI NA VICHEKESHO AKIVAA FLANA ILIYOANDIKWA KENYA,SIJUI,NAUOMBA MNIELEWE SINA UHASAMA NA MAJIRANI ZANGU BUT KIHALISI NINGETEGEMEA KUONA TANZANIA ZAIDI KAMA MWAKILISHI WETU,HEBU TUJITAMBUE JAMAN MB0NA SIO JAMBO GUMU SANA HASA UKIZINGATIA SAFARI YENYEWE UNAHUSIANA NA ASILI YETU WATANZANIA AMBAO TUNAJIVUNIA NA LUGHA YETU THEN MWAKILI KAMA HUYU ANAKUWA HAJITAMBUI.TUBADILIKE

    ReplyDelete
  6. AnonymousJuly 01, 2013

    NYIE MBONA MNA TSHIRT ZIMEANDIKWA USA?

    ReplyDelete
  7. AnonymousJuly 01, 2013

    jamani musimlaumu sana nikutojuwa nini anakifanya mpaka hapo alipo hajajuwa chochote kile ..elimu ni kitu kimoja kizuri na huyu mtu ni zero kwenye kichwa chake

    kufika usa sio sababu

    ReplyDelete
  8. AnonymousJuly 01, 2013

    Acheni uchelema wa akili nyie. Ile ni t-shirt ya kawaida tu kama zilivyo t-shirt zingine!

    ReplyDelete
  9. AnonymousJuly 01, 2013

    Watanzania kweli tumekosa utaifa, T-shirt ya Kenya nje ya nchi, what is that? Kavaa mradi kavaa pasipo kuangalia yuko wapi na anaitangaza vp nchi ya Kenya na si Tanzania.

    ReplyDelete
  10. AnonymousJuly 01, 2013

    ni ujinga ujinga tu! Kenya????

    ReplyDelete
  11. AnonymousJuly 01, 2013

    Hili jinga kabisa hili! badala ya kutangaza nchi yako unakengeuka! Ubiishiiii tu!

    ReplyDelete
  12. AnonymousJuly 01, 2013

    hapo thamani yake imeshuka sababu anaonekana hana utaifa kabisaa.WaTZ wengi hawana utaifa mpaka raisi wetu maana leo kwny ugeni wa OBAMA wimbo wamataifa ulipokuwa ukipigwa OBAMA anaweka mkono kwenye kifua kuashiria upendo wa nchi yake kwa moyo wake wote ilihali mwenyeji wake hafanyi hivyo kuonyesha uzalendo wa nchi.

    ReplyDelete
  13. AnonymousJuly 01, 2013

    Masanja jifunze na rekebisha haraka sana la sivyo next time utajikosesha mialiko kwa kuvaa vitu vya wenzetu, mana hapo huonyeshi ucommedian hata kidogo bali ni kuidharau nchi yako ya Tanzania. Shilole msaidie mwenzio mueleze aelewe asilete utani.

    ReplyDelete
  14. AnonymousJuly 02, 2013

    Nyie wote munaomulaumu Masanja Mwanawani ndiyo munautindio wa ubongo. Masanja hakwenda nje kutangaza utalii. Kazi yake kubwa ni kufanya watu wacheke au wawe na gumzo, na kwa kuvaa Kenya wakati anatoka TZ tayari keshafanya kazi yake. Ama mukatae au mukubari hivyo ndivyo ilivyo.

    Anony mmoja kasema juu ya elimu. Binafsi sijui kiwango cha elimu ya masanja, lakini ninataka kukuhakikishia anony kuwa wachekeshaji wote huwa ni genous, na wanamuziki maarufu pia. Kwa hiyo anony usilee ujinga kwa kudhani kuwa akili ni kumaliza chuo kikuu. Je, waliohitimu vyuo vikuu kwa vyeti vya kuchonga unasema nini juu yao! Wana akili kama yako, sio?

    ReplyDelete
  15. AnonymousJuly 02, 2013

    Pengine Wakenya ndiyo waliyo mfadhili! Ataachaje kucheza ngoma yao!
    Wa Tz sisi ni pungufu katika uzalendo wetu. Hakuna mwenge ahueni pamoja na mimi! Sababu za mapungufu hayo ziko nyingi. Mosi. Tunafuata nyayo za Viongozi wetu bila kufikiri, kutafakari na kuchambua kisha kuto maamuzi magumu.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...