Familia ya Marehemu Constantine L.Mavere wa Tabata Chang’ombe Dar Es Salaam,inatoa shukrani kwa wote walioshiriki kwa namna moja au nyingine kumuuguza mpendwa wetu Constantine hadi alipofariki Dunia Tarehe 21.06.2013 na kupumzishwa katika nyumba ya milele Tarehe 24.06.2013 huko Kondoa.
Ni vigumu kuwataja wote lakini shukrani za pekee ziwaendee :
1.Madaktari na wauguzi wa Kinondoni Hospital (Kwa Dr.Mvungi) na kwa namna ya pekee Dr.Ally Mwanga.
2.Watumishi wa kiroho (Mapadre) Parokia ya Kristu Mfalme Tabata DSM na Parokia ya Mt. Paulo wa Msalaba Kondoa.
3.Msajili na wafanyakazi wa Mahakama ya Biashara
4.Majirani,Ndugu,Jamaa na Marafiki wa Dar Es Salaam,Dodoma,Arusha,Singida na Kondoa.
Familia inawakaribisha kwenye Ibada ya Misa ya shukrani itakayofanyika nyumbani kwa Marehemu Tabata Chang’ombe Dar Es Salaam Tarehe 03.08.2013 saa 5.00 asubuhi.
KARIBUNI SANA
BWANA ALITOA, BWANA AMETWAA JINA LAKE LIPEWE SIFA
AMEN
mungu amrehemu marehemu. mimi nimezaliwa dar na kukulia dar mhhh lakini tabata changombe mimi kwa kweli sipajui. naomba nifahamishwe ni wapi
ReplyDeleteRest in Peace my Inlaw. Mdau wa kwanza Tabata Changombe unashuka kituo kinaitwa Barakuda then unaenda kulia, zipo pia daladala zimeandikwa Tabata Chang'ombe, Kuzaliwa Dar it doenst guarantee you to know every corner of the city.
ReplyDelete