Na Dixon Busagaga,wa Globu ya Jamii Moshi.
TIMU ya taifa ya Tanzania Taifa stars imerejea leo jioni nchini
ikitokea Uganda ambako ilikuwa na mchezo wa marejeano wa kufuzu
kucheza fainali za wachezaji wanaochjeza ligi za ndani (CHAN)
Kikosi hicho kimerejea majira ya saa 10:00 Jumapili jioni na ndege ya Precision
na kutua katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kilimanjaro ambako
walipokelewa na viongozi mbalimbali wa chama cha soka mkoa wa
Kilimanjaro.
Msafara wa timu hiyo uliondoka uwanjanai hapo na kuelekea katika hotel
ya Nyumbani iliyopo mjini Moshi ambako kulikuwa kumeandaliwa chakula
na mapumziko kabla ya kwenda kupanda ndege kurejea jijini Dar es
salaam.
Hata hivyo licha ya kipigo cha bao 3 kwa 1 kutoka kwa timu ya Uganda
mashabiki wa soka katika mji wa Moshi walijitokea katika hotel hiyo
kusalimiana na wachezaji huku baadhi wakionesha kusikitishwa na
matokeo hayo.
Wachezaji wa Stars wakiwa wamepumzika nje ya hotel ya Nyumbani mjini Moshi.
Wachezaji wa Stars.
Meneja wa timu ya Taifa Leopord Tasso Mukebezi akitambulisha mashabiki wa Stars kwa wachezaji wa timu hiyo.
![]() |
Wachezaji wa Stars wakiingia kwenye gari tayari kuelekea uwanja wa ndege KIA kurejea jijini Dar es salaam. |
sasa mmimi nahisi team ya Taifa stars ivunjwe kabisaaaaaa, halafu ziwekwe sura mpya, hawa washazoea kufungwa kwa hio sidhani tena kama watakuja fanya mabadiliko.
ReplyDeletehebu wahusika wekeni sura mpya kabisa kuanzia golikipa hadi watu wa ufundi.
maana hakuna jipya tena taifa stars.
Kufungwa twafungwa ila chenga twawala.
ReplyDeletehii timu ni ya wazembe tuu..wana wadhamini chungu nzima na pesa nzuri wanapewa lakini matokeo ni zero...ivunjwe tu waje wachezaji wapya...hawa hamna kitu nw!!
ReplyDeletecha kwanza hapo sie Tanzania tutaendelea kupoteza pesa nyingi kwa ajili ya kuwalipa makocha wa kigeni wakati wachezaji tulionao walishazeeka yaani mishe mishe za kukimbizana kiwanjani hawawezi misuli imezeeka,sana halafu wanakula vibaya wanakula viuzri tu wakiwa kambini sasa hapo timu hamna ,siku timu ikitengenezwa ndio vizuri ndio kocha wa kigeni atafutwe la sivyo tutakuwa tunapoteza hela.kuwa na kocha mzungu sio kuwa na timu nzuri tuangalie tunapokosea kwanza baadae ndio hawa watu watafutwe kwa jili ya kupanga wachezaji ambao walishaandaliwana sisi,sio kuwa na kocha mzungu basi tunaweka miguu juu ,itakuwa inakula kwetu kila mwaka.
ReplyDelete