
Waziri wa Fedha Dkt.William Mgimwa na Mwenyekiti na Rais wa Benki ya Export Import ya Korea wakisaini mkataba wa mkopo kwa ajili ya kujenga vituo vya kuhifadhi vitambulisho vya Taifa leo jijini Dar Es Salaam.

Waziri wa Fedha Dk.William Mgimwa na Mwenyekiti na Rais wa Benki ya Export Import ya Korea wakiangalia mikataba ya mkopo baada ya kusaini kwa ajili ya kujenga vituo vya kuhifadhi vitambulisho vya Taifa leo jijini Dar Es Salaam.

Waziri wa Fedha Dk.William Mgimwa (kushoto)akimpa mkono wa shukrani Mwenyekiti na Rais wa Benki ya Export Import ya Korea baada ya kusaini mkataba wa mkopo kwa ajili ya kujenga vituo vya kuhifadhi vitambulisho vya Taifa leo jijini Dar Es Salaam.

Waziri wa Fedha Dk.William Mgimwa kushoto akiwa na Mwenyekiti na Rais wa Benki ya Export Import ya Korea wakionyesha mkataba wa mkopo wenye thamani ya shilingi billioni 87 za kitanzania,waliosaini kwa ajili ya kujenga vituo vya kuhifadhi vitambulisho vya Taifa leo jijini Dar Es Salaam.

Waziri wa Fedha Dk.William Mgimwa akitoa neno la shukrani kwa niaba ya Serikali ya Tanzania kwa Mwenyekiti na Rais wa Benki ya Export Import ya Korea baada ya kusaini mkataba wa mkopo kwa ajili ya kujenga vituo vya kuhifadhi vitambulisho vya Taifa leo jijini Dar Es Salaam.Picha zote na Lorietha Laurence-MAELEZO
Ni muhimu Vitambulisho vya Taifa vikaharakishwa ili TUWEZE KUTAMBUANA NI NANI MTANZANIA NA NANI SI MTANZANIA.
ReplyDeleteHII LICHA YA KUHARAKISHA MAENDELEO YETU ITATUSAIDIA ZAIDI KTK HUU MCHAKATO WA KUELEKEA AFRIKA YA MASHARIKI.
Inaonyesha wazi hivi sasa Utanzania unazidi kuwa na thamani KTK HII AFRIKA YA MASHARIKI licha ya kuwa wengi wetu hatujui.
Eti ni mkopo wa kuwatafutia wananchi viatambulisho???? si watumie tu vya kupigia kura halafu hiyo hela iwekwe kwenye elimu na afya! Raha kweli kutia sahihi ya mkopo!
ReplyDelete