Familia ya Mzee Shilatu wa Mbagala wanasikitika kutangaza kifo cha Baba yao Mpendwa JOHN SHILATU kilichotokea katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili tarehe 23/07/2013 saa 10 jioni kutokana na shinikizo la damu.
Habari ziwafikie Ndugu, Jamaa, Marafiki, Viongozi, Wanasiasa wote wanaomfahamu vyema Marehemu popote pale walipo.
Mipango ya mazishi inafanyika Nyumbani kwa Marehemu Mbagala. Kwa mawasiliano zaidi juu ya msiba piga simu namba 0717 488622
Bwana alitoa na Bwana ametwaa, Jina la Bwana lihimidiwe.
Amen!!


Mwalimu Shilatu Mwalimu mkuu chang`ombe RIP.
ReplyDeleteNa mimi namkumbuka nilivyoanza darasa la kwanza yeye nod alikuwa mwalimu mkuu.......RIP mwl Shilatu
ReplyDeleteMwalimu Shilatu, Mungu akuweke mahali pema peponi. Familia ya Shilatu na wanafunzi wote Mwl. Shilatu aliyewaongoza poleni sote.
ReplyDeleteMwenyezi Mungu amlaze mahali pema peponi Mwalimu John Shilatu. Ninamkumbuka akiwa Mwalimu Mkuu wa Chang'ombe Primary School na ile mitihani yake ya kila Jumatano na Ijumaa na kiwango cha kufaulu alichokiweka cha 70% kwenda Juu.
ReplyDeleteAlitusaidia sana na hatimaye Chang'ombe Primary School ilipeleka wanafunzi 51 Shule za Sekondari Tanzania nzima.
Mwalimu Shilatu, Mwenyezi Mungu akulaze mahali pema peponi.
Amen,
Wafiwa poleni sana.
Mungu Amlaze Mwalimu Shilatu mahala pema. Ni Mwalimu Mkuu aliyemaintain status ya Chang'ombe Primary kuwa top kwa muda mrefu.
ReplyDeleteRIP Mzee wetu,ulikuwa baba mwema na mwenye upendo
ReplyDeleterest in peace our beloved head teacher chango'mbe primary 1980 nilipoanza darasa la kwanza!! MELCHIOR KULWA GASPER
ReplyDeleterest in peace our beloved teacher by melchior kulwa gasper
ReplyDeleteRIP Mwalimu wangu ulinifundisha mimi na binti yangu na tulifika mbali kwa msingi wako mzuri wa ufundishaji
ReplyDelete