Familia ya Mzee Shilatu wa Mbagala wanasikitika kutangaza kifo cha Baba yao Mpendwa JOHN SHILATU kilichotokea katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili tarehe 23/07/2013 saa 10 jioni kutokana na shinikizo la damu.
Habari ziwafikie Ndugu, Jamaa, Marafiki, Viongozi, Wanasiasa wote wanaomfahamu vyema Marehemu popote pale walipo.
Mipango ya mazishi inafanyika Nyumbani kwa Marehemu Mbagala. Kwa mawasiliano zaidi juu ya msiba piga simu namba 0717 488622
Bwana alitoa na Bwana ametwaa, Jina la Bwana lihimidiwe.
Amen!!

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 9 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 24, 2013

    Mwalimu Shilatu Mwalimu mkuu chang`ombe RIP.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 24, 2013

    Na mimi namkumbuka nilivyoanza darasa la kwanza yeye nod alikuwa mwalimu mkuu.......RIP mwl Shilatu

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 24, 2013

    Mwalimu Shilatu, Mungu akuweke mahali pema peponi. Familia ya Shilatu na wanafunzi wote Mwl. Shilatu aliyewaongoza poleni sote.

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 24, 2013

    Mwenyezi Mungu amlaze mahali pema peponi Mwalimu John Shilatu. Ninamkumbuka akiwa Mwalimu Mkuu wa Chang'ombe Primary School na ile mitihani yake ya kila Jumatano na Ijumaa na kiwango cha kufaulu alichokiweka cha 70% kwenda Juu.

    Alitusaidia sana na hatimaye Chang'ombe Primary School ilipeleka wanafunzi 51 Shule za Sekondari Tanzania nzima.

    Mwalimu Shilatu, Mwenyezi Mungu akulaze mahali pema peponi.

    Amen,

    Wafiwa poleni sana.

    ReplyDelete
  5. AnonymousJuly 24, 2013

    Mungu Amlaze Mwalimu Shilatu mahala pema. Ni Mwalimu Mkuu aliyemaintain status ya Chang'ombe Primary kuwa top kwa muda mrefu.

    ReplyDelete
  6. RIP Mzee wetu,ulikuwa baba mwema na mwenye upendo

    ReplyDelete
  7. AnonymousJuly 24, 2013

    rest in peace our beloved head teacher chango'mbe primary 1980 nilipoanza darasa la kwanza!! MELCHIOR KULWA GASPER

    ReplyDelete
  8. AnonymousJuly 24, 2013

    rest in peace our beloved teacher by melchior kulwa gasper

    ReplyDelete
  9. AnonymousJuly 24, 2013

    RIP Mwalimu wangu ulinifundisha mimi na binti yangu na tulifika mbali kwa msingi wako mzuri wa ufundishaji

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...