Leo mnamo saa 11:30 asubuhi vichwa viwili vya treni ya huduma la jiji la Dar es Salaam vilipata ajali ya kugongwa na roli la mizigo aina ya Fusso katika makutano ya reli na barabara ya Kawawa jijini Dar es salaam , katika jali hiyo dereva wa Fusso alifariki duniani papohapo hata hivyo Utingo wake alinusurika.

Hata hivyo vichwa hivyo vya treni vilipata mkosi tena wa ajali ambapo viligongwa na basi dogo la Daladala aina ya Isuzu katika makutano ya reli eneo la Kamata. Tukio hilo lilisababisha majeruhi kadhaa katika basi hilo la daladala ambapo majeruhi  wamelazwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbil wakiwemo askari wawili Polisi kutoka Kikosi cha Reli  mmojawapo akiwa  mahututi.
 
Vichwa hivyo viifanikiwa kufika stehesheni kwa wakati na kuanza kutoa huduma ya usafiri wa treni jijini  kutoka Dar Stesheni kwenda Ubungo Maziwa hadi saa 5 asubuhi hata hivyo huduma ya leo  jioni Julai 01, 2013, imesogezwa mbele na itaanza saa 12 jioni badala ya saa 10:30 alasiri. 

mabadiliko haya yamebidi yafanyike   kufuatia Jiji la Dar es Salaam kuwa na hekaheka ya kumpokea Raisi wa Marekani Barack Obama.
 
Aidha uongozi wa  TRL unawataarifu wakazi wa jiji kuwa kesho Julai 02, 2013, huduma za treni ya jiji hazitakuwepo hadi keshokutwa Julai 03, 2013, ambapo zitaendelea kama kawaida.
 
Imtolewa na Afisi ya Uhusiano kwa Niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa TRL,
 Mhandisi Kipallo Aman Kisamfu.
 
Makao Makuu ya TRL
Dar es Salaam.
Julai 01, 2013.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 01, 2013

    Hizi ajari kati ya treni na watu/magari zimekuwa zikitokea mara kwa mara jijini DSM, kuna jitihada zozote za TRL za makusudi kupunguza ajari hizi? au ndo tunaendela kuishi kumungu mungu tu

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 01, 2013

    Mdau hata mie pia nilikuwa najiuliza swali hilo hilo. Mie naona hizi treni haziendeshwi na wajuzi kabisaa, zinaendeshwa na watu wanao otea otea tu yaani wanabahatisha maana ajaali za treni zimekuwa nyingi sasa!!! Ni bora mtu kupanda basi tu hakika.

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 01, 2013

    ajari ,ajari.

    Kama hujui kiswahili kwani ni lazima kutoa maoni?

    ReplyDelete
    Replies
    1. AnonymousJuly 02, 2013

      Nimecheka. Unawafundisha kiswahili mbona kazi unayo salsa looh!

      Delete
  4. AnonymousJuly 02, 2013

    Kwa kawaida mahali ambapo reli inavuka barabara huwa kuna viashiria ambavyo huonesha na kutoa tahadhari iwapo treni inakuja,hivyo basi gari haziruhusiwi kupita mpaka treni ipite na itoke ishara salama yenye kuruhusu gari kupita.Sina hakika kama viashiria hivyo vipo huko nyumbani na kama vipo je vinafanya kazi?Mbali na hilo la viashiria, hawa madereva wetu wa siku hizi hawana tahadhari wao ni kuwahi tu na hicho ndicho kinachowafanya wasababishe ajari mara kwa mara, naamini kwa utaratibu huu wa viashiria vya usalama penye makutano ya reli na barabara ukizingatiwa hakuna ajari itakayo tokea kizembe.Nakumbuka makutano ya reli pale kamata, buguruni,tandika zamani sana nikiwa bado nipo TZ kulikua na viashiria na madereva wengi wa enzi hizo walikua wasikivu na wenye kutii.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...