Ankal akiwa katika sebule ya nyumba aliyokuwa akiishi Mzee Nelson Mandela Mtaa wa Vilakazi namba 8115 huko Orlando ya Magharibi, Soweto, Afrika Kusini. Hii ilikuwa Julai 18, 2010 wakati wa kuadhimisha Hepi Besdei ya miaka 92 ya kuzaliwa kwa Madiba. Leo Globu ya Jamii inaungana na wadau wote duniani kuadhimisha miaka 95 ya shujaa huyu wa Afrika anayependwa na kila mtu.
Ikumbukwe pia kwamba leo ni siku ya Kimataifa ya Mandela kama ilivyotangazwa na Umoja wa Mataifa mwaka 2011.
Tunamtakia aendelee kupata nafuu na aweze kuinuka kitandani huko hospitali alikolazwa kwa mwezi mmoja sasa ili apulize mishumaa yake na kukata keki huku sisi tukimwimbia HAPPY BIRTHDA MADIBA!!!!
Yafaa sote tujiulize iwapo kuna kitu jamii itatukumbuka kwacho hapo uzeeni. Ona kila mtu anampenda na kumwona Madiba kama Babu yake. Tutende mema jamani.
ReplyDeleteHappy Birthday Baba Mandela! Nakutakia maisha marefu mengine na M/Mungu akupe ahueni ya haraka katika maradhi yako.
ReplyDeleteKatika siku ya leo ni MANDELA DAY, na pia nashukuru kuwa leo ni siku yangu pia ya KUZALIWA!
Najivunia sana tarehe na mwezi wa kuzaliwa kwangu kuwa sawa na wewe Mheshimiwa Mkuu wa Dunia.
"HAPPY BIRTHDAY TO US"=Nelson Mandela + Peters Mhoja!