Imekuwa ni mazoea kwa jamii yetu kupuuza na
kutokuzipa uzito kauli na mawazo yanayolenga kujenga taifa letu. Badala yake
tumekuwa tukitumia muda mwingi kushabikia na kuongelea mambo yasiyo na tija kwa
taifa. Kwa sababu hii CHADEMA UK tuko mstari wa mbele kuzipigia mbiu na kuzipa
umuhimu na uzito wake kauli za waTanzania zenye nia ya kulijenga taifa tukianza
na kauli nzito iliyotolewa na Shekh Mkuu wa Baraza la Waislamu nchini
(BAKWATA).
Kwanza kabisa Tunampongeza kwa dhati kabisa kwa ujasiri mkubwa
kuzungumzia maswala mabayo viongozi wetu wengi katika ngazi mbali mabli
kitiaifa wanalikwepa aidha kwa makusudi au kutokana nan nidhamu ya uoga. Shekh
Shaban Simba amegusia swala muhimu sana kuhusiana na mustakabali wa siasa na
dini ndani ya nchi yetu. Kwa uwazi mkubwa na kwa nia njema kabisa katika juhudi
za kuliepusha Taifa letu na migangano ya
kiimani katika misingi ya malumbano ya kisiasa, ametutahadharisha WaTanzania
wapenda amani kuwa makini na baadhi ya wanasiasa wanaojenga utamaduni wa
kupenyeza siasa katika nyumba za ibaada kwa kasi kupitia iilimradi wapate
majukwaa ya kuendeleza matakwa yao ya kisiasa.
Na zaidi ameelezea mpango wa
kuanzisha vikundi vya usalama ili kulinda amani ndani ya BAKWATA.
Hivi karibuni tumeona jinsi ambavyo baadhi ya
wanaiasa wamejikita kwenye nyumba za kuabudu kwa kile ambacho ni dhahiri katika
kuendeleza (to pursue) ndoto zao za kisiasa. Cha kusikitisha ni kwamba baadhi
ya viongozi hawa kwa nyakati tofauti wameshawahi kuhikilia nyadhifa mbali mbali
za kisiasa na ndani ya serikali.
Kwenye nyadhifa zao ungetegemea wangetumia
nafasi zao kuonesha ufanisi na na kudhihirisha uwezo wao wa kuongoza na kujenga
imani kwa wananchi. Badala yake wanatumia nyumba za kidini kutaka tena nafasi
za kuongoza. Cha kusikitisha zaidi ni jinsi ambavyo baadhi ya viongozi wa dini
wanavyokubali kurubuniwa na kutumiwa vibaya na wanasiasa. Alichozungumzia Shekh
Mkuu ni ukweli usiopingika kwamba nyumba za dini si majukwaa ya kisiasa.
Kama
waTanzania wenye mapenzi na nchi yetu, tunapenda kusisitiza na kukazia kauli ya
Shekh Mkuu. Nyumba za kuabudu zitumiwe kwa madhumuni hayo na si vinginevyo.
Shekh Mkuu pia ametoa agizo la kuundwa kwa kamati
za ulinzi ndani ya BAKWATA nchi nzima ili kulinda amani. Alisema mpango huu ni
katika kutekeleza maagizo yaliyopendekezwa na kiongozi mkuu wa jeshi la Polisi
nchini IGP Said Mwema. Nia ni kugundua viashiria vya uvunjaji wa amani na
kuzipeleka kwenye vyombo vinavyohusika.
Kwa mukhtasari tu, IGP ametoa maelekezo
haya kwa kuwa uwezo wa jeshi la Polisi kulinda na kuzuia matukio ya kijangili
ni mdogo na hauwezi kufika kila mahali hivyo ni jukumu la viongozi wa taasisi
mbali mbali kuweka mikakati ya ulinzi kwenye mikusanyiko yao. Kwa mantiki hii
Shekh Mkuu ana kila sababu ya kujipanga na taasisi nyingine zina kila sababu ya
kujipanga.
Ni jambo la ushujaa na lenye kuonesha ukomavu
kuona kiongozi mkuu wa dini akiweka bayana hisia zake kuhusu mustakabali wa
siasa na dini ndani ya nchi. Na kwa sababu hiyo CHADEMA UK tunampongeza Shekh
Mkuu kwa kuonyesha mfano wa kuigwa na viongozi wote wa dini kukemea bila staha
utamaduni huu wa kujaribu kuingiza siasa katika nyumba za ibada.
Kila kiongozi
angekumbuka wajibu wake kama shekhe Shaban Simba, tuna imani kuwa mambo mengi
ya kijami yaliowashinda wanasiasa kukemea kwa kukosa (moral authority), yange
fanyiwa kazi kwa ufanisi kwa wale wanoaminiwa na jamii kwa kiwango kikubwa.
CHADEMA UK itaunga mkono kwa nguvu zote MTanzania yeyote atakaye simamia msingi
mikubwa ya amani kitaifa kama Shekh Shaban Simba. Kwa upande wa kauli ya IGP
kuhusu vikundi vya ulinzi katika taasisi mbali mbali, tuna kila sababu ya kuamini kwamba
mapendekezo haya ya IGP kuwataka viongozi wa taasisi mbali mbali kuanzisha
vikundi vya ulinzi ili kusaidiana na vyombo vya dola katika kulinda
mikusanyiko yao , yamekuja wakati muafaka hasa baada ya kiongozi huyo mkuu
kukiri uwezo mdogo wa Polisi katika kulinda amani nchi nzima.
MUNGU IBARIKI TANZANIA
CHADEMA UK
Hivi Watu mpo UK mnawaza siasa za Tanzania .Mtakuwa na njaa Kali sana huko .Pigeni Mzigo huko mke ku invest Tanzania siasa itawafikisha wapi ?.Poleni njaa
ReplyDeleteMm ci CHADEMA wala CCM,ila kwa haya maneno yenu wallah tupo pamoja,,mfano huyu EDWAD mmasai apingwe kwa njia zote anapenda sana mambo ya udini udini mara kachangia waislam mara kachangia wakilisto hii ni dalili mbaya kabisa katika jamii yetu,sote kwa pamoja tuseme noo bila ya kumuonea aibu aiache TANZANIA ichanue kwa AMANI,ni mm mdau wenu mpenda amani,nipo mji wa LEICESTER,UK mungu ibaliki TZ.
ReplyDeleteNatamani CHADEMA UK ndio wangekuwa CHADEMA nzima.
ReplyDeleteManeno yzenu ni mazito yaliyoshiba busara na upeo.
Nina wasi wasi kama kweli nyie ni CHADEMA halisi. Au mnawasaliti wenzenu?
Sisi wabongo huku ughaibuni tuksikia na kuona kauli za viongozi wa CHADEMA kule nyumbani mara zote huwa zimelenga katika kauli mbiu ya chama chenu: NCHI HAITATAWALIKA! Na kweli, maana vurugu zote za miaka ya karibuni CHADEMA ndio kiini.
Ndio nikauliza hapo juu nyie ni CHADEMA gani mnaosisitiza upendo na masikilizano?
Au mmebadilika?
Au mwawasaliti viongozi wenu?
Mndengereko, Ukerewe
Chadema hawajatulia.From my experience Watu wengi walio USA Chadema wanawivu mnoo na watoto SA viongozi huko Tanzania .wanawasemaga vibaya Nakumbuka kuna kiongozi alistaafu miaka iliyopita na Chadema waliofanya party kubwa Kwenye apartment na Kusema watamwona BINTI yake ataishije hapo USA .chakushangaza Yule BINTI anapiga Mzigo masaa 14 kila siku 7 days .Mtoto Huyo wa kiongozi huyo anajituma haswa wao Chadema nyama china kila siku kazini hawapendi .mimi nikajiuliza why wanawasemaga Hawa watoto wa viongozi ? Nikashtukia wivu .Ukiwa profile utawaona Chadema wengio walio nje ya nchi hawana kazi washaharibu credit na ni wapo wapo tu .Na Hawa soon walio nayo Chadema ni warudi Tanzania kuanzisha fujo.
DeleteShekh mkuu Shaban Simba nakuomba ushirikiane na viongozi wengine wakuu wa dini mkomeshe ujinga ulioshamiri kwenye uongozi wa serikali ya taifa letu Tanzania. Kwa ujasiri wako utatusaidia kuokoa hili taifa. Kwa sasa serikali ya Tanzania imelala usingizi fofofo AMA imekufa. Itakuwaje viongozi wa serikali wanakuwa matajiri wakubwa kwa kipindi cha muda mfupi tu, itakuwaje elimu imekufa na viongozi wanasomesha watoto wao shule za private, inakuwaje viongozi wanatibiwa nje ya nchi na walalahoi hawana hata maji safi ya kunywa, inakuwaje kiongozi wa serikali anapenyeza kwenye taasisi za dini na kuchangia mabilioni ya shillingi, inakuwaje mabomu yanalipuka makanisani na kwenye mikutano ya hadhara na wananchi hawapewi tarifa kujua kinachoendelea, inakuwaje kiongozi wa taasisi nyeti anatekwa nyara na kuteswa na wananchi hawapewi tarifa yeyote, n.k., n.k., ...... Baba sheikh mkuu, hili taifa letu linakwenda wapi?? Tafadhali kwa nafasi yako ambayo Mungu amekupa, na kwa nafasi yako kwenye jamii, tafadhali simama imara utusaidie kuokoa hili taifa.
ReplyDeleteKwa sasa hivi serikali ya Tanzania Haina uongozi. We are simply floating around like a lost ship. Hakuma kiongozi mwenye uwezo wa kuchukua maamuzi mazito na kutoa muelekeo wa taifa. We are simply lost. Sasa inabidi sheikh mkuu aingilie kuliokoa taifa. Asante sheikh mkuu Shaban Simba. I support you 100%.
ReplyDeleteImetulia sana Mkuu na ujumbe umefika. Ni watu MUFILISI ndio wanaofanya vuti kama hivi na cha ajabu viongozi wetu wa dini wanashabikia!
ReplyDeleteHawa ni watu hatari sana ktk jamii!
Safi kabisa Mdau nimeipenda sana hii! midahalo wanaikimbia wanakwenda makanisani na misikitini kuwarubuni wachungaji na masheikh NJAA. Ebo!
ReplyDeleteTatizo kubwa tulilonalo ni la usiri na pia kutoangalia masuala yetu kisayansi. Nikisema kisayansi namaanisha ukweli/haki. Unajua ukiwa unafanya kila kitu ku--generalize ni vigumu sana kutatua tatizo lolote. Mfano neno "uchochezi", "udini", "ukabila", "kukashifu" n.k. yakiwa yanatumika kwa kusema tu mfano: wachochezi wote wa dini watachukuliwa hatua kali. Sasa hapa kama hujaweka maana halisi nini uchochezi unaleta masihara. Kwa sababu kila upande atachukua maana ya uchochezi kwa kadri nafsi yake inavyoona.
ReplyDeleteWanasiasa wanaweza kwenda kwenye taasisi za dini. Kama nilivyoeleza hapo juu maana ya dini haijaeleweka kwa Watanzania. Kwa Tanzania "dini" inaweza kufikiriwa kwamba ni uislamu,ukristo,ubudha,na uhindu.
Lakini kwa uhalisia wake dini maana yake ni mfumo wa maisha wowote binadamu kajichagulia. Mfano kama wewe mfumo wako wa maisha ni kama mkusanyo wa haya yafuatayo: {kuingiliana kimwili na jinsia yeyote, kunywa pombe, muziki, kwenda kanisani/msitini/hekalu, kula chakula cha aina yeyote, kufanya kazi ya kujipatia kipato ya aina yeyote ile, n.k.}, dini yako itakuwa ni hiyo ambayo tunaweza kuiita dini "X". Kwa sababu mkusanyiko wa matendo hayo hapo haifanywi na dini tunazozizoea.
Na tunaona wanasiasa wanatumia wanamuziki/wanakwaya kwenye siasa, na hawa nao ni aina ya dini yao. Kwa hiyo kwa tafsi ya haraka ni kwamba dini haiwezi kukwepeka. Kwa sababu kila kitu ni sehemu ya dini fulani. Hata kama utasema unaweza kukwepa hata si uhalisia.
Kuna nchi za Ulaya zinasema usichanganye dini na siasa; lakini na waongo wakubwa. Uingereza mkubwa wa nchi ni malkia ambaye ni mkubwa wa anglikana. Na kama nilivyoeleza hapo juu maana halisi ya dini ni ivo ivo katika nchi za ulaya. Mfano ujerumani madangulo yako ya kumwaga waweza kwenda kujivinjari unavyotaka. Maana yake ni kwamba huo ndio mfumo wa maisha ya hao wajerumani na hiyo ndiyo dini yao.
Kwa maelezo ya hapo juu miye niko tofauti na mufti na niko tofauti na nakala hii. Nataka haya yafuatayo yawe ndiyo msingi wa taifa letu:
(1) Watu wote wawe huru katika siasa; maana yake ni kwamba wanasiasa waende makanisani waende misikitini waende kwenye mahekalu kuomba kura za kuwa kiongozi wa kuongoza Tanzania. Cha msingi ifanyike kwa uwazi manake sasa hivi yaweza fanyika kwa siri jambo ambalo si la kweli.
(2) Anayechaguliwa kuongoza Tanzania ajali haki ya kila raia bila ubaguzi wa aina yeyote. Haki ya kupata elimu mpaka ashindwe mwenyewe, haki ya kufanya kazi kwenye ajira yeyote, haki ya kupata matibabu kwa ugonjwa wa aina yeyote, haki ya kuishi kwenye nyumba bora, haki ya kuabudu kwa uhuru kulingana na misingi ya dini yake/vitabu vyake, haki ya kupata mlo bora,n.k.
(3)Waliowekwa madarakani kwa namna yeyote wasineemeshe/pendelea dini yeyote ili kuiwezesha hiyo dini kustawi kuliko nyingine. Au kudhoofisha dini hiyo kwa mtindo huo. Au kumbadilisha mtu dini kwa kumlaghai kwa kumpatia huduma ya jamii, hela, n.k. Mtu atabadili dini baada ya kukiniishwa misingi ya dini husika na si vinginevyo.
(4) Watu wasome dini zingine ili kujua misingi ya hizo dini. Hii itaongeza kuvumiliana. Mfano: kama wakristo vitabu vyao vinawaleza wavae rozari, basi watu wa dini nyingine wamvumilie huyu anayevaa rozari; na kama waislamu kwa mujibu wa vitabu vyao vinawaelekeza kuvaa hijabu basi wenye dini nyingine wawavumilie wote wanaovaa hijabu. Kwa mtindo huu ndiyo tutaitwa "WATANZANIA WALIOELIMIKA" na amani ya nchi haitayumba kabisa.
(4) Ni kama namba tatu hapo juu, ni msisitizo tu. Nchi yetu iandae maukumbi/facilities kuhakikisha kwamba wananchi wawe wanakutana hapo na kila dini ieleze dini yao ipoje na kwanini iko tofauti na zingine. Kwa mtindo huo tutakuwa na taifa linalojitambua na si kwenda bila kuwa na uelewa wa mambo.
Kila la kheri
UK!!!!!!!!??? Mnnnh Rudini bongo kwanza halafu ndio tusikilize mnachosema! Mkiongelea UK kama mnagelesha vile! na kuvishana vilemba vya ukoka acheni utani!!!
ReplyDeleteAsanteni CHADEMA UK,naona upeo wa elimu na pia wa siasa.Mtatusaidia sana. Tatizo ni la viongozi kukaa kimya na kukubali kila jambo baya,(kinyume kabisa na ahadi zao za kuombea kura. Mfano, pale waziri mkuu aliposema bungeni kwamba polisi wawapige wananchi na wabunge wote wakapiga makofi,ilitosha kabisa kujua kwamba hatuna wawakilishi isipokuwa mbunge mmoja tu wa Zanzibar aliyesema kwamba hiyo ni kinyume cha katiba na makinda akaizima kauli yake. Lakini cha muhimu,na ninaomba ikiwa mtaweza kuliongelea hili,nchi nyingi sana mabadiliko yabaletwa na asasi zisizo za ki-serikali(NGOs) Hivi NGOs za Tanzania ni za serikali?hivi ni lini zinaongelea masuala ya kijamii,hivi lini tumesikia zikiongea redion ana tv kukemea uvunjaji wa haki za binadamu, rushwa, elimu duni,na kero zingine?Nashawishika kusema kwamba NGOz za Tanzania 'ni za serikali' na hazina msaada kwa jamii. Suala lingine ni uhuru wa vyombo vya habari, haviko huru na habari tunazosoma ni za kutafuta kwa bidii na kwa tabu sana yale mazuri ambayo serikali imefanya. Tunaona nchi zingine ambapo watu wanaanika ripoti ya fedha zilizotumika kutengeneza nyumba ya rais na watu wanatoa comments bila wasiwasi wa kupotezwa.Nitaendelea badae.
ReplyDeleteUk ni masaa saba tu, Mwaza ni masaa mangapi?. Kuwa nje si sababu ya kutoshiriki kujenga nchi ulikotoka.
ReplyDeleteNa kama IGP ameruhusu ulinzi wa taasisi mbalimbali basi ina maana brigades za rangi zote ruksa, sio?