Kiongozi wa ujumbe kutoka ubalozi wa Marekani hapa nchini Bw. Jeff Shrader akitoa shukrani zake kwa uongozi na wafanyakazi wa TTCL alipotembelea makao makuu ya Kampuni hiyo.
Afisa Mkuu wa Mauzo na Masoko wa TTCL Bw. Peter Ngota akiwashukuru wawakilishi kutoka ubalozi wa Marekani hapa nchini kwa kutambua mchango wa TTCL katika kufanikisha ziara ya Rais wa Marekani alipotembelea Nchini Tanzania.
Afisa Mtendaji Mkuu wa TTCL dkt. Kamugisha Kazaura akipokea cheti cha shukrani kutoka kwa Kiongozi wa ujumbe kutoka ubalozi wa Marekani hapa nchini Bw. Jeff Shrader.
Afisa Mtendaji mkuu wa TTCL Dtk. Kamugisha Kazaura akibadilishana mawazo na Kiongozi wa ujumbe kutoka ubalozi wa Marekani hapa nchini Bw. Jeff Shrader.
Uongozi wa TTCL pamoja na wawakilishi wa Ubalozi wa Marekani hapa nchini katika picha ya pamoja.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 25, 2013

    TTCL dume!

    Kwa kweli Shirika limekomaa, ni kuwa pana wengine walitutisha ohhh Ujio wa Raisi Obama mawasiliano yatakuwa hayapatikani, Ohhh Kadi za ATM hazitafanya kazi,ohhh intaneti itakuwa na kasi ya chini.

    Mbona mambo yalikuwa shwari tu, si mnaona jinsi TTCL na TCRA zilivyo jipanga?

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 26, 2013

    Lakini TCRA msaada wao kwa wateja wenye mitandao wakiboa ni mdogo sana. Hata ukiwapa nakala ya barua sidhani kama utapata utambulisho wa kuipokea na kusikilizia. Wenye mitandao wakikujibu hawatoi nakala TCRA na kwao wao sio tatizo. Mimi ukinambia nilinganishe TCRA na mamlaka nyingine ya ufutiliaji kama EWURA mimi nitakwambia kwangu EWURA ni bora maana nina mfano wa msaada kutoka kwao. TCRA secretary ndio anjua zaidi ndo maana hata sasa siridhishwi na picha za king'amuzi flani lakini najiuliza mara mbili ama niwasiliane na TCRA au wizara maana msaada wao kwangu umejitokeza kuwa haupo. Wamejipanga sana ndio maana watu walisajili simu zao miaka mitatu ilipita na kuwa na vielelezo siku za karibuni bado walitumiwa ujumbe wa kuwataka wapitie kwenye maofisi ya kampuni husika wakamilishe usajili. Kwa kifupi wamejipanga.


    sesophy@gmail.com

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 26, 2013

    na hao waliokaa hapo viti vya mbele mbona wamekaa kizembe sana? tafuteni picha nzuri kuweka kwenye blog, shirika kubwa but hawa walitakiwa wafundishwe itifaki

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...