IMG_9991
Mshauri wa Radio Jamii kutoka UNESCO Rose Haji Mwalimu akifafanua umuhimu wa mafunzo hayo ya Ujasiriamali kwa Redio za kijamii kwa washiriki ambayo yatawajengea uwezo wa kuboresha vipindi vyao na kufanikisha kupata wadhamini ili kumudu gharama za uendeshaji wa vituo vyao. Warsha hiyo imeshirikisha radio 9 za jamii zinazotekeleza mradi wa kuziwezesha Redio hizo masuala ya TEKNOHAMA unaoratibiwa na Shirika la UNESCO chini ya udhamini wa SIDA. Warsha hii ni mwendelezo wa mafunzo ya Ujasiriamali katika Redio za jamii chini ya mradi huo.
IMG_0061
Mshauri Mwelekezi masuala ya utawala bora Bw. Wilbert Kitima akiendesha mafunzo kwa washiriki wa Redio Jamii yanayofanyika Kayanza, Karagwe Bukoba.
IMG_0017
Pichani juu na chini ni baadhi ya washiriki kutoka Redio za jamii 9 ambazo zinazotekeleza mradi wa SIDA unaoratibiwa na Shirika la UNESCO nchini wakichangia mawazo yao namna ya kutengeneza mpango mkakati wa biashara kwa ajili ya kumudu gharama za uendeshaji wa Redio zao.
IMG_0069
IMG_0065
Washiriki wakiendelea kupata mafunzo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. ArchitectJuly 16, 2013

    Asante kaka kwa kutuhabarisha. Masahihisho kidogo.Mji huo unaitwa KAYANGA na si Kayanza. Pia wilaya ya Karagwe..haiko Bukoba bali iko Kagera. Maana Bukoba ni Wilaya nyingine ya mkoa wa kagera si kwamba Karagwe iko ndani ya Bukoba.asante kaka

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...