Na Woinde Shizza,Arusha 

Wachimbaji wadogo wa madini ya Tanzanite wa Mji mdogo wa Mererani Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara wameiomba Serikali kuipatia leseni kampuni ya kizalendo ya Tan Youth Mining Ltd,ili wauziwe zana za milipuko kwa bei nafuu.

Wakizungumza leo mbele ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini chini ya Kaimu Mwenyekiti wake Anne Kilango Malecela,wachimbaji hao walisema kampuni hiyo ikipatiwa kibali na kufutiwa kodi watachimba madini kwa urahisi.

Mmoja kati ya wachimbaji hao,Sokota Mbuya alisema kampuni hiyo chini ya Mkurugenzi wake,Mohamed Karia ingepatiwa kibali cha kuwasambazia wachimbaji wadogo zana za milipuko wangekuwa na unafuu mkubwa.

“Kwanini mzalendo asipewe kibali cha kutusambazia zana,apewa mtu wa South Africa,ambaye hatusaidii chochote yaani inatusababisha twende hadi Nairobi Kenya kufuata zana za milipuko ya migodi,” alisema Mbuya.

Hata hivyo,Kamishna Msaidizi wa madini kanda ya kaskazini,Benjamin Mchwampaka aliieleza Kamati hiyo kuwa kwa alishaidhinisha kampuni hiyo ipatiwe kibali hicho,ila kinachokwamisha ni makao makuu wizarani.

“Kampuni hiyo ingeweza kuwasaidia wachimbaji wadogo kwa suala la milipuko na nilishasaini yote yanayonihusu,ila wizarani bado hawajasaini na alishahojiwa mpaka na kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa ,” alisema Mchwampaka.

Akizungumzia kuhusu hilo,Kaimu Mwenyekiti wa kamati hiyo,Anne Kilango Malecela aliwataka wachimbaji hao kuandika barua kwenye kamati hiyo wakutane na wizara mwezi ujao ili kampuni hiyo ipatiwe kibali hicho.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 08, 2013

    Duu!! Serikali iwaangalie wachimbaji hawa kwani ni kati ya utajiri tulio nao hapa nchini Tanzania! Inakuwaje wasi saidiwe na wao wajikomboe na waendelee kuikomboa Tanzania yetu. Wanafanya kazi katika hali ngumu na mazingira duni sana.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 09, 2013

    Haki tena hela yatafutwa namna hii! halafu kibaka anakuja kuikwapua!

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 09, 2013

    Uncle naomba urushe mawazo yangu kwa Wadau kuhusu namna ya kuboresha Sekta ya Madini hususani wachimbaji wadogo.

    Nikiwa ni Mtanzania mwenye mapenzi mema na taifa nionapo vijana wakitanzania wanajituma kusaka note kwaajili ya familia zao na kwa uchumi wa taifa basi mimi huwa nasisimukwa (I become emotional).

    Ombi langu kwa Serikali ni kuwa hawa vijana walioko katika sekta ya uchimbaji mdogo wa madini warasmishiwe shughuli zao kwa kuwaandikisha ktk vikundi, wapewe mafunzo na lesseni na wakopeshwe vifaa vyakisasa.

    Serikali inaweza kufanya hili ikiamua maana si suala gumu.Naomba Mamlaka inayosimamia Sekta husika na Viongozi wa ngazi ya juu wenye maamuzi walione hili nakulifanyia kazi.

    How and where to find money?

    Option 1: Serikali inaweza kukopa hata World Bank kwa kutoa sababu yakutaka kurasimisha wachimba madini wadogo na kuwapatia vitendea kazi ili waweze kuwa na ufanisi ili wachangia pato la taifa.

    Option 2:Serikali inaweza kuanzania mfuko (Trust Fund) utakao changiwa na Wawekezaji na wanunua madini nchini kwa tozo la asilimia ndogo sana labda tusena asilimia 0.5 au less kwa thamani ya jiwe. Hili tunaweza kulittetea na hata kufuatilia hata huko kwenye masoko ya madini e.g New York Commodity Market Exchange yanako nadiwa madini yetu kabla hata hayachimbwa wakati siye hata kodi hatulipwi vizuri wakati serikali yao inapata kodi yote. From ethical and Social Corporate Responsibility linauzika vizuri, kwanza hiyo hela inarudi kwenye kuboresha sekta husika na hivyo kuongeza productivity suala ambalo ni zuri.Tena kwenye blog hii leo nimeona taarifa inayosema Serikali imesaini makubaliano ya ushirikiano wa kidau na AngloGold Ashanti na Barrick hapo ndio pakuanzia sasa yasiwe tu makubaliano ya kwenye makaratasi ambayo hayatusaidii.

    Option 3:Wanunuliwe vifaa na kopeshewe na Serikali kutoka katika vyanzo vingine vya Serikali na wakatwe kila wanapofanya mauzo kidogo kidogo hata kwa miaka ishirini ijayo. Suala hili litasaidia kuwa na Sector economic player wakitanzania ambao hela yote watayopata inabaki nchini wakati kipato chao kinaimarika.

    Wahusika naomba tuondokane na mawazo mgando maana hayasaidii taifa letu kusonga mbele kiuchumi. Sekta ya madini ni moja ya Sekta ambazo zinaweza kulibeba taifa letu kwa haraka kutoka kuitwa the pooret economy, it is a shame and sounds very bad kwa taifa lenye rasilimali kama Tanzania.

    Ushauri wa jumla: Serikali iamue kugharmia kuwasomesha vijana tena waliomaliza tu darasa la saba, form four au six (not degree)utaalamu wa uchimbaji madini kwa kuanzisha program maalumu katika Veta. Ikumbukwe Afrika Kusini enzi za mkoloni sekta kubwa iliyokuwa imewajiri weusi tena mpaka kutoka nchi jirani za msumbiji, Botwasana na Zimbabwe ilikuwa ni uchimbaji wa madini. Hivyo,hii ni sekta moja kubwa ambayo inaweza kusaidia kutatua tatizo la ajira kwa kwa vijana wengi kuliko tunavyoiona.

    Asante msomaji kwa kutafakari mawazo yangu.

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 11, 2013

    Michuzi!
    Nimefurhishwa na mawzo ya mdau alietoa maoni hayo hapo juu. Napenda utafute namna ya kuwapelekea wadau tuchambue kwakina suala la wacchimbaji wadogo ili lipate bufumbuzi wakudumu. Kama mchango wako kwa taifa nivema upatapo mawazo mazuri ukakusanya nakuwapelekea wahusika kwa hatua zao.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...