Mfanyabiashara mmoja ameuwawa na majambazi walokuwa wakitumia usafiri wa pikipiki maarufu kama Boda Boda huko Magomeni Mapipa jijini Dar es salaam, karibu na makutano ya mtaa wa Jaribu na Tosheka milango ya saa 4 asubuhi tarehe 19 July, 2013 siku ya ijumaa na kumpora pesa taslim millioni 8 na laki 3. 
Tukio hilo limetokea nyumbani kwake barazani akiwa ametoka bank kuchukua pesa hizo na kuvamiwa na majambazi hayo. Mfanya biashara huyo mwenye asili ya kiarabu anaitwa Abdul Hakim Salmin na alikuwa maarufu sana katiko maeneo hayo. 
 Marehemu amezikwa katika makaburi ya Kisutu na ameacha mke na watoto watano, sasa tunajiuliza je jeshi la polisi liko wapi? Tunaomba serikali ifuatilie na kupanga mkakati jinsi ya kuwalinda wananchi wake. Jee wana usalama wako wapi kwani kila mara matukio ya kuporwa wafanyabiashara na wengine kupoteza maisha na hizo boda boda. 
Jeshi la polisi au askari polisi wengi wanaoutumia pikipiki , maarufu kama 'TIGO FASTA', utawakuta kibao maeneo ya jangwani wakifatilia magari (pick up) zinazoleta mizigo inayosafirishwa mikoani kutaka risiti na kama hamna basi huwa wanadai kitu kidogo ili upite. 
Kwa kweli ukiwaona hao mapolisi wanaotumia pikipiki wanavyolizunguka jangwa ni vituko vikubwa, sisi kama wananchi tunajiuliza je wamepewa hayo mapikipiki kwa kazi hiyo au kulinda raia na mali zao? Wadau wa Magomeni Mapipa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 21, 2013

    Mimi nadhani kuna haja ya askari polisi kukagua piki piki zote hasa kujua hao wanaotumia pikipiki kama hawajabeba silaha.
    Jamani mbona tunapoteza raia wengi kwa hao majambazi wanaofanya hujuma bila hata kuogopa chochote tena mchana. Enyi majambazi hamjui ipo siku mutahukumiwa, kuna Mungu anayeangalia matendo yenu maovu,mnawaacha watoto yatima na wajane, acheni kuua watu. Si heri kama mngekuwa mnapora tu hizo pesa pasipo kuua watu. Mnamwaga damu isiyo na hatia mnadhani Mungu haoni. Acheni hiyo tabia tubuni dhambi zenu ili msamehewe.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 22, 2013

    Labda swali la kujiuliza vipi walijua katoka kuchukua pesa? kama kuna watu wanacheza na tigo pesa na kutoa taarifa za watu wanaochukua pesa nyingi kupitia tigo pesa then kuna mtu a ndaniya tigo anatoa hizo taarifa...nadhani watu watazame ndani ya tigo nani kaprocess pesa zake huyu mfanyabiashara kuanzia hapo tutajua wapi pa kuwapata...

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 22, 2013

    R.I.P, Inasikitisha sana, yaani mimi naogopa hata kuja likizo huko home maana hata pa kupita palipo salama hakuna, watembea huku watu wakikuangalia na kukufuatilia,humjui yupi mzuri yupi mbaya, usalama umekua wa mashaka mtupu,sijui hao polisi wanajishughurisha na nini? siasa?Utawaona kibao kila walipo CDM,Uchawi mtupu,raia wanateseka tu, ebu ona mzee wa watu amekwenda ameacha watoto.

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 22, 2013

    MAJAMBAZI WANAFAHAMIKA NA WANANCHI. HATA HIZO PICK PIKI ZINAFAHAMIKA NA RAIA WENGI TU. JAMBO KUBWA HAPA NI KUWA WANASHIRIKIANA NA BAADHI YA HAO ASKARI....KWA MFANO HAI..HIVI KARIBUNI KIJANA MMOJA ALINYANGANYWA PIKI PIKI NA KUUMIZAWA VIBAYA SANA. ASKARI WA KITUO CHA KAWE WAMEBADILISHA MASHTAKA NA KUWA NI KUUMIZWA TU NA SIO WIZI WA PIKIPIKI?????? HUYU KIJANA AMEWATAJA WALIOMDHURU NA KUMNYANG'ANYA NA ANAFAHAMIKA HATA MTAANI KUWA NI MWIZI WA PIKIPIKI ILA POLISI WALA HAWAMFANYII UPELELEZI WA SIRI. HATA UKITAKA KUPELEKA TAARIFA UNAONA NOI USUMBUFU. PIA SEHEMU AMBAZO NI CHACHE SANA ZENYE MATUKIO KAMA HAYA YANGEWEKEWA CAMERA MBONA UHALIFU UNGEPUNGUA?? DAWA NI KUCHAGUA CHAMA KINGINE TUUU

    ReplyDelete
  5. AnonymousJuly 22, 2013

    Hao polisi mwenye pikipiki kazi yao ni kutafuta hongo tu wamefanya hizo pikipiki kuwa ni mradi wao nadhani wanatakiwa kupeleka hesabu kila siku

    ReplyDelete
  6. AnonymousJuly 23, 2013

    WADAU NAONA TUNASEMA SANA NA TUNAANDIKA COMMENTS AMBAZO KILA MMOJA ANAONYESHA VIPI TUNAATHIRIKA NA MAMBO HAYA.SWALI NI JEE HIZI HABARI ZINAWAFIKIA WALENGWA???
    JEE NI HATUA GANI WENYE MADARAKA WAMECHUKUA???KWA KADIRI NINAVYOJUA TUNA MAKAMANDA WA KILA AINA TZ KAMA VILE KAMANDA WA UPELELEZI,WA JINAI, WA USALAMA WA RAIA NA WENGI TU NA WOTE WANAWAFUASI KWA MAMIA.
    INASIKITISHA SANA KWAMBA HAWA WATU HAWAFANYI KAZI ZAO KABISA NA ETI WANAAPISHWA NAKUSEMA WATAFANYA KAZI ZAO KWA UADILIFU NA KULINDA RAIA.
    KWA KWELI RAIA INABIDI TUJIDHATITI NA KUDAI HAWA VIONGOZI NA WANAUSALAMA JINA KUWAJIBIKA -AMA SIVYO TUTAMALIZWA,NA TUACHE KUDANGANYA KUWA TZ KUNA AMANI - NI AMANI GANI MTU ANAULIWA NA KUNYAN'G'ANYWA HAKI YAKE?NA VIPI TANZANIA ITABARIKIWA KAMA IKIWA VIONGOZI HAWATENDI UADILIFU?VIONGOZI HAYA NI MAJUKUMU YENU NA MTAKUJA KUULIZWA MBELE YA ALLAH.
    HILI TATIZO LA MAJAMBZI LINAOTA MIZIZI NA WANAUSALAMA NDIO WANOPALILIA.KWA NINI HAWAPELELEZI NA KUYAKATA MIZIZI?NI VIPI LEO WANAPATA SILAHA?HAKUNA HATA TAASISI WALA DUKA MOJA TANZANIA YENYE KUDHIBITI AU KUUZA SILAHA ISPOKUWA JESHI NA POLISI.
    HILI NI TATIZO SUGU NA NI LAZIMA VIONGOZI TOKA RAIS MPAKA CHINI NI LAZIMA WALIFANYIE KAZI.
    KUNA HABARI ZA CHINI KWAMBA HAWA MAJAMBAZI WANAPATA TIP TOKA KWA WATU WA BENKI NI RAHISI TU HAWA WATU KUFANYIWA UCHUNGUZI KWA KWANZA KUKAGULIWA SIMU ZAO AU HATA KUZIMONITOR.PIA WASIACHIWE WAKIWA KAZINI KUTUMIA SIMU KWA KUWABONYEZA MAJAMBAZI.
    INASIKITISHA NA KUSIKITISHA NDUGU ZETU WANAVYOTOLEWA ROHO ZAO KWA AJILI YA MALI ZAO.
    NA TUTASIKITIKA SANA KAMA HATUJASIMAMA KIDETE NA HAO MAKAMANDA JINA.
    JESHI LA POLISI TAFADHALINI SANA HAO TIGO FASTA WAAFUATILIENI WAFANYE KAZI ZAO KULINDA RAIA NA SIO KUKAMATA WANYONGE WASIO NA RISITI AU WENYE MAGARI YASIYOKUWA NA TRIANGLE HIYO SIO KAZI YAO.
    RAIA TUJUMUIKENI NA TUWAKATE NISHAI HAO TIGO FASTA NA TUSIKUBALI WATUTESE.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...