Kamishna Mkuu wa Magereza Nchini Zambia, Percy Chato( Suti ya rangi ya maziwa) akimsikiliza Muongozaji wa Watalii anayeelezea kama anavyoonekana wakati walipotembelea Ngome Kuu ya Sultani iliyokuwa ikitumika kama Kituo Kikuu cha Watumwa kabla ya kusafirishwa kwenda Zanzibar. Gome hii ipo Mji Mkongwe Bagamoyo, Mkoa wa Pwani na imejengwa Mwaka 1889 na Warabu ambao ndo walikuwa wanafanya Biashara ya Watumwa hapa nchini Tanzania( wa kwanza kulia) ni Kamishna wa Sheria na Uendeshaji wa Magereza ambaye aliongozana na Ujumbe huo wa Viongozi wa Magereza toka Nchi Wanachama wa SADC, Dkt. Juma Ally Malewa.
Kamishna Mkuu wa Magereza Nchini Zambia, Percy Chato( Suti rangi ya maziwa) akiangalia Mnara ambao umejengwa sehemu ambayo Wajerumani wakitumia kunyoongea Waafrika ambao walikuwa wanawaunga Mkono Warabu enzi hizo. Mnara huo umejengwa mwaka 1868 na Wajerumani, anayeelezea ni Muongozaji wa Watalii na wanaangalia ni baadhi ya Maafisa kutoka Makao Makuu ya Jeshi la Magereza Tanzania.
Kamishna wa Sheria na Uendeshaji wa Magereza, Dkt. Juma Ally Malewa akiangalia Sefu ya kutunzia Pesa ambayo ipo katika Makumbusho ya Kanisa Katoliki la Bagamoyo, Mkoa wa Pwani. Wengine wanaangalia ni Makamishna Wakuu wa Magereza toka Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika wakati walipotembelea Makumbusho hiyo leo.
Kamishna wa Sheria na Uendeshaji wa Magereza Nchini, Dkt. Juma Ally Malewa( wa kwanza kulia) akiwa na Makamishna Wakuu wa Magereza wa Nchi za Zambia(mwenye Suti ya rangi ya maziwa) na Kamishna Mkuu wa Magereza Nchini Msumbiji(mwenye kofia) walipotembelea Ngome Kuu ya Sultani iliyoko Bagamoyo, Mkoa wa Pwani na ilitumika kuwahifadhi Watumwa enzi za Biashara ya Watumwa hapa Nchini kama unavyoweza kuona katika picha lango Kuu la kuingilia Vyumba vya kuwahifadhi Watumwa enzi hizo. Wengine katika picha ni Maafisa Waandamizi kutoka Makao Makuu ya Jeshi la Magereza Tanzania(Picha na Lucas Mboje wa Jeshi la Magereza).

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 23, 2013

    Hayo majengo mbona yataanguka, yanatakiwa kufanyiwa ukarabati ambao hauta badili taswira ya asili. Jamani akin Nyalandu huko vipi au ndio tunaweza tu kuongea kwenye ma tv kazi hatuwezi. Hiyo historia itapotea na Bagamoyo location Ni very strategic. Watalii wanateremka tu halo airport kituo cha kwanza tunawapeleka Bwagamoyo wanaacha michuzi, safari inaendelea. Yaani kweli kwenye miti mingi hakuna wajenzi nimeamini.

    ReplyDelete
  2. Kwa inavyosemekana jina halisi la mji huo lilijulikana kama 'BWAGA MOYO', ispokuwa liliathiriwa na ujio wa wageni nyakati hizo (watawala), hivyo kutokana na ugumu wa lugha na utamkwaji wake, wakaishia kutamka na kupaita BAGAMOYO, ndio mpaka leo hii.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...