Naibu Kamishna Jererali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Luteni Kanal LS Mgumba amewapandisha vyeo Maafisa pamoja na Askari mbalimbali wa Jiji la Dar Es Salaam kwa niaba ya Kamishna Jenerali.

Upandishwaji wa vyeo hivyo ulifanyika Julai 19 saa nne asubuhi katika ukumbi wa Mikutano wa Chuo cha Jeshi hilo.

Upandishwaji wa vyeo hivyo umefinyika kwa kuzingatia sheria Na.14 ya Jeshi la Zimamoto na Uokoaji ya mwaka 2007, Kanuni ya Jeshi la Zimamoto na Uokoaji ya mwaka 2008 pamoja na Muundo wa Utumishi wa Jeshi hilo. Sheria ya Jeshi la Zimamoto na Uokoaji inatamka na kutambua Mamlaka ya upandishwaji vyeo kwa upande wa Maafisa iko ndani ya Tume ya Utumishi ya Polisi na Magereza ambayo ilijadili na kupitisha Maafisa wa Jeshi la Zimamoto na Uokoajikwa vyeo tofauti.

Upande wa Askari wa ngazi ya chini kuanzia Koplo mpaka Sameja mamlaka ya upandishwaji vyeo iko chini ya Kamishna Jenerali wa Jeshi hilo.

Akiongea na Askari waliopandishwa vyeo Kamanda Mgumba aliwataka Maafisa na wapiganaji kutoridhika na viwango vya elimu walivyonavyo na kusisitiza wajiendeleze zaidi ili kuongeza ufanisi na utendaji kazi. 

 Aliendelea kusema:- “Kutonana na teknolojia mpya ya uzimaji moto ni vyema mjiendeleze ili kuendana na mabadiliko ya teknolojia na kuongeza msingi na mwenendo wa kazi za Askari ni nidhamu, utii ukakamavu, uvumilifu na uzalendo hivyo ni lazima kwa maafisa na Askari kuwa na nidhamu na huo ndio msingi wa kazi za kijeshi ikiwa ni pamoja na kujituma, hiyo ndiyo asili ya mafanikio ndani ya Jeshi”.

mwisho Naibu Kamishna aliwapongeza sana Maafisa na Askari walipandishwa vyeo na aliwasisitiza kutumikia vyeo hivyo kwa uadilifu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...