Meneja Mawasiliano wa shirika la nyumba la Taifa Bw, Yahaya Charahani
akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati ambapo
waandishi hao walitembelea eneo la kibada wilaya ya Temeke kujionea
Nyumba 3 zinazoshindaniwa katika promosheni ya Airtel Yatosha. Nyumba
hizi zimenunuliwa na Airtel toka shirika la nyumba la taifa kwaajili
ya promosheni ya AIRTEL shinda Nyumba.kulia ni Meneja Uhusiano wa
Airtel Bw, Jackson Mmbando
Meneja Uhusiano wa Airtel Bw Jackson Mmbando akiongea na waandishi wa
habari (hawapo pichani) wakati ambapo waandishi hao walitembelea eneo
la kibada wilaya ya Temeke kujionea Nyumba 3 zinazoshindaniwa katika
promosheni ya Airtel Yatosha. Nyumba hizi zimenunuliwa na Airtel toka
shirika la nyumba la taifa kwaajili ya promosheni ya AIRTEL shinda
Nyumba 3.
Mwishoni mwa wiki hii Shirika la nyumba la taifa limewathibitishia
watanzania kwamba tayari nyumba tatu zinazoshindaniwa katika
promosheni ya airtel yatosha zimekamilika na tayari mafundi wanafanya
matengenezo ya mwisho tayari kwa kukabidhiwa kwa washindi hao.
Afisa Uhusiano wa NHC YAHAYA CHARAHANI amesema hayo mwishoni mwa wiki
wakati ambapo wanahabari toka vyombo mbali mbali walitembelea nyumba
hizo kujionea jinsi mradi unavyokwenda
“nyumba hizi tatu zenye thaman ya shilingi milioni 194 zimekamilika na
pindi washindi watakapotangazwa wataweza kuhamia katika nyumba hizi
mara moja tu.
Amesema nyumba hizo ambazo ni za kisasa zitakidhi mahitaji ya wengi
kwani ujenzi wake umezingatia mahitaji ya familia kubwa.
Nyumba hizi zina vyumba vitatu vya kulala, jiko, sebule nzuri pamoja
na sehemu ya nje iliyonakishiwa kwa umakini ili kuipa nyumba mvuto wa
hali ya juu. Aliongeza bw, CHARAHANI
Pia alibainisha kuwa wateja wa kampuni ya airtel wanaweza kuzitembelea
nyumba hizo na kujionea wenyewe kiwango cha ubora wa nyumba hizo.
“Hizi nyumba ziko wilaya ya Temeke eneo la kibada karibu kabisa na
Tuangoma ambapo hadi kufika katika nyumba hizi ni umbali wa kilomita 2
tu kutoka kituo cha basi kilipo, eneo ambalo linafikika na linamakazi
mzuri sana” alimalizia kwa kusema Bw, CHARAHANI.
Nae Meneja Uhusiano wa Airtel JACKSON MMBANDO amewataka watanzania
kuendelea kutumia mtandao wa airtel hususani huduma ya yatosha kwa
kupiga *149*99# na kuchagua vifurushi vinavyowatosha ili
kujihakikishia nafasi ya kushinda nyumba hizo.
Amesema airtel imedhamilia kutatua matatizo ya wateja wake kwa kutoa
huduma nafuu na bora kuliko mtandao wowote lakini pia promosheni hiyo
ya YATOSHA inalenga kubadilisha maisha ya watanzania hasa wale
wanaotumia mtandao wa airtel
Amesema katika promosheni hiyo jumla ya shilling million 284
zitatumika kuwazadia wateja wa kampuni hiyo ambapo milioni 194
zitanunua nymba hizo 3 toka shirika la nyumba na kiasi kinachobaki kwa
siku 90 Airtel itatoa milioni moja kwa mshindi mmoja kila siku.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...