Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb.) akizungumza masuala mbalimbali katika kuimarisha ushirikiano kati ya Tanzania na New Zealand alipokutana na Waziri wa Mambo ya Nje wa nchi hiyo Mhe. Murray McCully tarehe 22 Julai 2013. Mhe. McCully na ujumbe wake wapo nchini kwa ziara ya kikazi ya siku mbili tarehe 21  na 22 Julai, 2013.
Mhe. McCully nae akimweleza Mhe. Membe masuala ya msisitizo katika kuimarisha ushirikiano baina ya nchi hizi mbili ikiwemo ushirikiano katika masuala ya biashara na kilimo.

Mhe. Membe na wajumbe kutoka Tanzania na New Zealand wakimsikiliza Mhe. McCully.
Mhe. Membe  akimkabidhi Mhe. McCully zawadi ya kinyago mara baada ya mazungumzo yao.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 22, 2013

    Very interesting..wasaidizi wa waziri wetu wanatumia iPAD lakini wale wa waziri wa New Zeland wanatumia karatasi...

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 22, 2013

    OMG, angalia tunavyojimaliza!! Wakati wageni wanaandika kwenye karatasi za kawaida, wenzangu (walioendelea kiteknologia) wemeweka mionzi mapajani, madhara yake tutayaona hivi karibuni. Natumaini hawa wameshamaliza mpango wa kuumba, otherwise..........

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 22, 2013

    anonymous 1
    kitu gani kimekushangaza hapa
    wasaidizi wa waziri wetu kutumia IPAD na watumishi wa waziri wa New Zealand kutumia karatasi?
    Kimtazamo ungetuandikia maoni ya waziri hon.B.Membe na serikali kwa ujumla kufanya vizuri katika maendeleo ya kuichumi na siasa za nchi za nje hadi kuwavutia mataifa madogo na makubwa kuja kuwekezea.
    mikidadi-denmark

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 22, 2013

    Anon July 22, 2013 wala usishangae sana sisi watu weusi umaskin wetu upo kwenye akili..hata tukienda shule hautoki unless labda tuishi na wenye utajiri wa akili kwa muda mrefu sana!

    Unashangaa hilo ndugu yangu??mbona hushangai magari V8 yaliyopo tele wakati wamama wanajifungulia sakafuni?tuna ile mentality ya ku-grab kila kitu kizuri kiwe chetu binafsi tu.

    J4
    Ujerumani

    ReplyDelete
  5. Ikingekua kinyume chake mngesema pia....fanyeni yenu acheni ku critize kila kitu

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...