Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiendesha pikipiki wakati alipozindua Mradi wa Pikipiki wa Kikundi cha SACCOS ya vijana wa Mbinga kwenye uwanja wa CCM mjini Mbinga akiwa katika ziara ya mkoa wa Ruvuma Julai 21, 2013.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akihutubia mkutano wa hadhara kwenye uwanja wa CCM mjini Mbinga akiwa katika ziara ya mkoa wa Ruvuma Julai 21, 2013.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda na mkewe Tunu wakizungumza na Mzee Andrea Mapunda (84) wakati alipotembelea shamaba la kahawa la mzee huyo katika kijiji cha Masumuni wilayani Mbinga wakiwa katika ziar ya mkoa wa Ruvuma Julai 21, 2013.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizindua mradi wa kupeleka umeme Mbambabay katika wilaya mpya ya Nyasa kutoka kwenye kituo cha kuzalisha umeme cha Mbinga akiwa katika ziara ya mkoa wa Ruvuma Julai 21, 2013. Kulia ni Mkewe Tunu na Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Thabiti Mwambungu. Watatu Kulia ni Naibu Waziri wa Nishati na Madini Stephen Masele.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiwapongeza baadhi ya waendesha pikipiki wa Mbinga baada ya kuzindua mradi wa pikipiki za kikundi cha SACCOS ya vijana wa Mbinga kwenye uwanja wa Mpira wa CCM mjini Mbinga akiwa katika ziara ya mkoa wa Ruvuma Julai 21, 2013. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 22, 2013

    mie nimeipenda kweli hiyo picha ya kwanza akiendesha pikipiki na kupigiwa makofi.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 22, 2013

    mimi nimependa kiwalo cha hao wanachama, jacket kwa ajili ya baridi ikiwa na reflective strip!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...