Home
Unlabelled
WAZIRI MKUU WA THAILAND Yingluck Shinawatra ATUA DAR LEO KWA ZIARA YA SIKU TATU
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Most read Swahili blog on earth
Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.
Akina dada mmeona hiyo?
ReplyDeleteMwenzenu ameshika usukani anaongoza nchi!
Wenzangu na mimi dada zangu akina Chausiki na Havijawa wa hapa Tanzania Bongoland kazi ni kuosha kucha, kusafisha miguu, Kubandika nywele bandia vichwani, kuogea na sabuni za Mikorogo, Kurushiana Mafumbo ya Mipasho kwenye Taarabu na kugombea wanaume na kutegemea Mabwana ktk kusukuma Maisha.
Tazameni mfano huo kwa wenzetu na ninyi mbadilike!
Kabinti kazuri kwelikweli.
ReplyDeleteKaka wa kwanza hapo juu umenena kweli ila jiandae kuchukiwa maana ukisema ukweli unaonekana mnoko
ReplyDeleteBasi dada Waziri Mkuu achia wafungwa wetu
ReplyDeleteMbona hamzungumzii idadi kubwa ya wanawake tena wenye uwezo katika madaraka na ngazi kubwa za mamuzi hapa nchini? Kweli Nabii hasifiwi katika Nchi yake. Mifumo dume bado ni kikwazo kwa wanawake wa Tanzania na Nchi nyingi zinazoendelea kushika usukani. Maraisi Ellen Johnson, Joyce Banda, mama Zuma AU just to mention a few. It a process & class struggle. Chungeni sana wimbi kubwa la mabadiliko halitaacha kuikumba Tanzania. Nini cha ajabu wanaume mmefanya Kama sio kuingiza Nchi katika ufisadi, ubinafsi na rushwa. TAFAKARI
ReplyDeleteBila shaka yule mdai aliyetoa ombi la matarumbeta ameburudika japo kwa kiduchu huku ombi lake likifanyiwa mchakato.
ReplyDeleteSawa mdau wa kwanza umesahau na wale wanaotaka VITI MAALAMU! Mwenzenu amegangamala hadi kuwa raisi hakuna mambo ya viti maalumu!
ReplyDeleteTunao kina Dr. Migiro,Prof. Tibaijuka etc. Tatizo ni jamii kukubali mwanamke kuwa rais, hata mataifa makubwa hiyo ni challenge.... nina hakika mdau wa kwanza upeo wako ni finyu sana.
ReplyDeletemdau wa kwanza anza na mkeo kwanza mpe madaraka uone kama hujahama nyumba ww
ReplyDeleteMataifa makubwa au taifa kubwa? Uingereza Margaret Thatcher, ujerumani Angela Merkel, hao wawili uliowataja hapo juu waliteuliwa UN hawakugombea km ckosei.
ReplyDeleteMhe: Yingluck Shinawatra a.k.a Pu
ReplyDeleteNi mama Mfanyabiashara na mwanasiasa. Ni Waziri Mkuu wa 28 ila ni kwanza Mwanamke tena mwenye umri mdogo.
ana miaka 46 (Juni21,1967); Ana urefu wa 1.7m (5'7"); ameolewa na ana mtoto mmoja. Anasadikiwa kuwa Mwanamke wa 31 kati ya akina mama wenye nguvu kimaamuzi na uluwa. Mwaka 2011 alikuwa na utajiri wa $ 17 Million (541 Million Baht); Mwanawe akiwa na 4.4 Million Baht na Mumewe akiwa na 76.8 Baht kwenye vifaa na 369.7 Million mtaji utokanao na madeni.