Mamia ya Waumini wa Karismatiki Katoliki Jimbo la Dar es Salaam wakiwa na mabango yenye ujumbe tofauti katika viwanja vya jangwani, jijini Dar es Salaam mara baada ya maandamano yao yaliyoanzia Msimbazi Centre hadi viwanja vya Jangwani kupokewa na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi katika Kongamano la Amani la kuiombea Tanzania.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi akiwa ameshika msalaba mara baada ya kupokea maandamano makubwa ya mamia ya Waumini wa Karismatiki Katoliki Jimbo la Dar es Salaam. Kushoto ni Mkurugenzi wa Idara ya Kushughulikia Malalamiko, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Augustine Shio.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi. Dk Emmanuel Nchimbi akizungumza na mamia ya Waumini wa Karismatiki Katoliki Jimbo la Dar es Salaam katika viwanja vya jangwani, jijini Dar es Salaam mara baada ya kuyapokea maandamano makubwa ya waumini hao yaliyoanzia Msimbazi Centre hadi katika viwanja vya Jangwani jana. Dk Nchimbi katika hotuba yake alisisitiza kuwa, atahakikisha viongozi wa dini ambao watafanya mihadhara ya chuki nchini kwa kuitukana dini nyingine watakamatwa na kufikishwa mahakamani. Picha zote na Felix Mwagara, Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 22, 2013

    Vizuri. Na kila mtu afanye jambo kama hili kwa vitendo na kutoka moyoni.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...