Waziri wa Maji,
Prof. Jumanne Maghembe (katikati) akiwa pamoja na baadhi ya wageni wa meza kuu
wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa tano wa
mwaka wa Bodi za Maji za Mabonde leo jijini Mbeya. Kulia kwa Waziri wa Maji ni
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Mhe.Abbas Kandaro.
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mhe. Abbas Kandoro akitoa
taarifa rasmi ya hali ya Maji Mkoani
Mbeya kwa wajumbe wa Mkutano wa tano wa mwaka wa Bodi za Maji za Mabonde (hawamo pichani) jijini Mbeya leo asubuhi.
Waziri wa Maji, Prof. Jumanne Maghembe akifungua
rasmi Mkutano wa tano wa mwaka wa Bodi za Maji za Mabonde leo jijini Mbeya.
Baadhi ya wadau wa sekta ya maji wanaoshiriki
Mkutano wa tano wa mwaka wa Bodi za Maji za Mabonde ulioanza leo jijini Mbeya.
Wadau wa sekta ya maji wanaoshiriki katika Mkutano wa
tano wa mwaka wa Bodi za Maji za Mabonde
wakiwa katika picha ya pamoja leo jijini Mbeya.
===== ====== ======
WAZIRI
WA MAJI AFUNGUA MKUTANO WA MWAKA WA BODI ZA MAJI ZA MABONDE JIJINI MBEYA.
Waziri wa Maji Pro.Jumanne Maghembe amefungua Mkutano
wa tano wa mwaka wa Bodi za Maji za Mabonde leo jijini Mbeya katika ukumbi wa Hoteli ya
Mtenda Sunset and Conference Centre.
Katika mkutano huo, Prof. Maghembe alisisitiza
kuweka mkakati wa utunzaji wa vyanzo vya maji na mazingira kwa ujumla, kwa
kuandaa mpango maalum wa taifa wa utunzaji wa vyanzo vya maji wa miaka mitano.
Pia, alishauri kuanzisha Mfuko wa Vyanzo vya Maji kwa
ajili ya jamii zinazoishi karibu na vyanzo hivyo, maalum kwa kuwezesha utunzaji
wa vyanzo hivyo ili kuhakikisha zoezi hilo linafanikiwa kwa ufanisi mzuri. Na
akapendekeza kiasi cha Sh. bil. 3-5 kwa kuanza mfuko huo.
Lengo la
mkutano huu ni kuwakutanisha wadau mbalimbali wa sekta ya maji ili kupitia
utekelezaji wa malengo na mikakati katika usimamizi na uendelezaji wa
rasilimali za maji kwa nia ya kuhakikisha kuwa rasilimali hizo zinatumika kwa
uwiano mzuri kwa sekta zote na kwa njia endelevu. Kauli mbiu ya mkutano wa mwaka huu ni “Jitihada za Pamoja katika Kutunza na
Kulinda Vyanzo vya Maji ni Muhimu ili Kuhakikisha Upatikanaji wa Maji.
Aidha, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji, Mha.
Bashir Mrindoko, aliongeza kuwa anategemea mbinu zaidi zitatumika katika kutekeleza
Programu ya Maendeleo ya Sekta ya Maji , ikiwemo njia ya usimamizi shirikishi
ili kupata ufumbuzi wa changamoto hizo.
Mkutano huo unategemea kuendelea mpaka tarehe 5,
Julai na utahusisha pia kutembelea vyanzo vya maji mkoani Mbeya, ambapo
kunapatikana karibu 70% ya vyanzo vya maji nchini.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...