Kutoka kushoto ni Paulyne Zongo, Khadija Mnoga (Kimobitel) na Joan Matovolwa. Wanamuziki hao watatu na wakongwe nchini ndio wanaounda kundi hilo litakalojulikana kwa jina la NDEGE 3.
 
Kundi la Ndege 3 linaloundwa na wanamuziki wakongwe katika Tasnia ya muziki wa dansi na kizazi kipya Joan matovolwa, Khadija Mnoga (Kimobitel) na Paulyne Zongo, hivi karibuni limeshatoa kibao chake kinachokwenda kwa jina la 'MISUKOSUKO YA MAPENZI' ambacho redio kadhaa nchini zimeanza kukirusha.
 
MISUKOSUKO YA MAPENZI ni nyimbo ambayo imetungwa kwa umahiri wa hali ya juu, na kuonyesha viwango vya juu katika uimbaji na utunzi.
 
Kwa sasa Joan Matovolwa na Paulyne Zongo ni wanamuziki huru wakati Khadija Mnoga (Kimobitel) ni mwanamuziki anayeimba katika bendi ya Extra Bongo inayoongozwa na Camarade Ally Choki.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 05, 2013

    Wow we shall support you ladies.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...