Global Publishers leo 7.7.2013 waliandaa Tamasha la Matumaini. Bahati mbaya sana sikuweza kuwahi kutokana na safari nilizonazo. Hii ni hotuba niliyopanga kuitoa na kuwatumia waandaaji.
TAMASHA LA MATUMAINI
Leo nilikuwa niwe nanyi kwa ajili ya siku hii muhimu sana kwa nchi yetu, siku ya matumaini kama inavyoandaliwa na Kampuni ya Global Publishers. Napenda kutoa shukrani zangu za dhati kabisa kwa ndugu yangu Erick Shigongo kwa kuandaa tamasha hili kila mwaka.

Nasikitika kuwa sitaweza kufanya pambano la ngumi na ndugu Ray na pia kuchezea timu yangu ya Wabunge wa Simba dhidi ya watani zetu Yanga. Hata hivyo naamini kuwa tamasha litakuwa na mafanikio makubwa na nipo nanyi japo sipo Dar es Salaam.
ZITTO KABWE.
Ilikuwa niwepo Dar es Salaam leo, lakini nimeshindwa kuondoka Marekani kwa sababu Spika wa Bunge Mama Anna Makinda ameniagiza kwenye safari nyingine ndefu kwenda visiwa vya Cayman na baadaye Namibia kwa shughuli za Umoja wa Wabunge wa Jumuiya ya Madola. Sikuweza kukwepa jukumu hili la kitaifa maana limekuja ghafla na mimi nipo huku jirani na maeneo hayo. Naomba radhi sana kwamba sipo nanyi leo.

Mhe. Zitto Kabwe,
ReplyDeleteTumekuelewa sasa kwa nini tusisogeze mbele tarehe badala ya 'kuchomoa' moja kwa moja?
Sasa hapo si ndio utasomeka ya kuwa umeweka GLOVU KWAPANI kumkwepa Mpinzani wako Ulingoni Ray?
Kama hamkuonana na Ray katika Saba saba tarehe 7.7.2013 Watanzania wangependa kukuona Mheshimiwa ukipanda Ulingoni kwenye NANE NANE yaani tarehe 8.8.2013
Tena muda huo utakuwezesha kupata nafasi huko Marekani kumpitia Mike Tyson ili akupe kwa uchache MBINU ZA USHINDI utakavyo mkabili Ray ukirudi Tanzania!
Au siyo?