Kwa hisani ya TFCA
Mahojiano haya yametokana na
-C. Sheria ya Ushuru wa Bidhaa, SURA 147
98. Mheshimiwa Spika, napendekeza kufanya marekebisho
katika Sheria ya Ushuru wa Bidhaa, SURA 147 kama ifuatavyo:-
ii. Mheshimiwa Spika, kumekuwa na kilio cha muda
mrefu cha wasanii kudurufiwa kazi zao za sanaa na
kukosa maslahi kwa kazi wanazofanya.
Ili kutatua tatizo
hili, Serikali kupitia Mamlaka ya Mapato itaanza
kurasimisha biashara ya bidhaa za muziki na filamu kwa
nia ya kuhakikisha kwamba uasili wake unatambulika na
hivyo kuzuia vitendo vya kudurufu kazi za sanaa (piracy of
artists work) hali ambayo inadumaza ukuaji wa sanaa na
vipaji hapa nchini.
Aidha, Mamlaka ya Mapato itaweka
stampu kwenye bidhaa hizo ili uuzaji wa kazi hizo uwe
rasmi na kuwawezesha wasanii kupata kipato stahili
kutokana na kazi zao. Vilevile hatua hii itaiingizia serikali
mapato.
80
Kwa kuwa yanahitajika maandalizi ya kutosha ikiwa ni
pamoja na kurekebisha sheria na kanuni mbalimbali,
utekelezaji wa hatua hii umeanza rasmi tarehe 1 Januari,
2013.
Tunaangalia uelewa wa wadau kuhusiana na hili na nini kifanyike ili kuweza kuboresha sheria husiaka ili iendane na taratibu na miongozo itakayoweza kuleta ukombozi wa kweli.


Hongera sana Dr. Shule na wote mlio toa hoja kwa umahiri sana, kuhusiana na masuala ya Filamu na Kodi.
ReplyDeleteDully Sykes, kwanza napenda kuanza kwa kusema kwamba nakuheshimu kama miongoni mwa wanamuziki wa mwanzo wa Bongo Flava, ambao mmechangia sana kuukuza mziki wetu huu tuuependao na hongera sana kwa kuendeleza mapambano mpaka sasa, kwani miaka 17 ya muziki si haba!
ReplyDeleteBaada ya hayo, ni muhimu nikaweka wazi kwamba maelezo yako katika mahojiano haya, yamenisikitisha sana, yaani unaonekana ni mtu wa lawama na kutaka kusaidiwa tu, bila kuwa tayari kubeba majukumu yako binafsi katika kuhakikisha maslahi yako yanalindwa.
Nazungumzia responsibility, ambayo haunyoneshi kuwa nayo, kwa mfano, haujui hata alama zinazotumika kulinda kazi zenu, na wala haujui kazi za wasanii zinalindwa vipi (wakati wewe ni msanii)???? Ukiulizwa kwanini, unasema "Mimi sijapata elimu yeyote na wala sikuitwa" sasa kwanini usifuatilie mwenyewe na kuweza kujielimisha na kujilinda? Maana mwisho wa siku, ni wewe ndio unayeibiwa na si BASATA wala COSOTA. Au ina maana ukongwe wako katika muziki huu na jina lako kubwa vina kuzuia kuwa fuata watu, mpaka ufuatwe au uitwe?
Amka Dully na wasanii wengine kwa kujielimisha wenyewe kwa kufuata hizo elimu zilipo na si kusubiri tu "kuelimishwa" na kusaidiwa na serikali na maadvocate!
Natambua kwamba mnafanya kazi katika mazingira magumu sana, maana wasanii wanashindwa kunufaika na kazi zao ipasavyo kutokana na wizi uliokithiri. Lakini, ufumbuzi wa tatizo hili hauwezi kupatikana bila wasanii wenyewe kuchukua jukumu la kujielimisha na kufuatilia mambo yote yanayohusiana na ulindaji wa kazi zao, kwani mhusika wa kwanza ni msanii mwenyewe. Kama msanii upo busy katika kufuatilia masuala haya, basi bila shaka upo busy unatengeneza pesa.
Kwahiyo basi, hakikisha kwamba una Meneja makini, ambaye atafuatilia masuala haya kwa niaba yako na baadae fursa ikipatikana mnakutana ili akuelimishe na wewe pia.
Ni ushauri wa bure tu.
Asanteni,
Rungwe Jr.
Hongera Rungwe Jr, maelezo yako ni mazuri sana, lakini sio Dully sykes tu au kwenye tasnia ya muziki tu, hata nyanja nyingine watanzania wengi badala ya kulitafutia utatuzi TATIZO, wao hubaki kulilalamikia TATIZO. wakijitahidi sana kulitatua basi inakuwa 'serikali itusaidie' kama vile kuna serikali ya kusaidia
ReplyDeleteMchangiaji wa kwanza Rungwe Jr umetoa somo tosha kabisa kwa wasanii wetu. Kwa kweli inasikitisha juu ya attitude yao ya kulalama kama watoto wadogo.Kuna wengine wanatengeneza pesa za kutosha wana magari zaidi ya moja na nyumba still wanataka Rais awasaidie matrekta!
ReplyDelete